Kipindi cha karibuni ni wazi umesikia kuhusu mvutano wa kibiashara uliokwepo kati ya marekani na china, mvutano ambao ulisababisha Raisi wa Marekani kutoa katazo la biashara kati ya kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ya Huawei na kampuni za Marekani.
Hata hivyo katazo hili lilisababisha kampuni nyingi za marekani kusitisha kufanya biashara na kampuni ya Huawei zikiwemo kampuni za Google, Qualcomm pamoja na Intel. Hata hivyo kusitishwa huko kwa biashara kulisababisha kampuni ya Huawei kukosa baadhi ya vifaa muhimu vya kutengeneza bidhaa zake kama vile smartphone pamoja na laptop zake mpya.
Sasa hivi karibuni habari mpya zinasema kuwa Raisi wa Marekani Donald Trump, kupitia mkutano wa G20 alisema kuwa ameruhusu tena kampuni ya Huawei kufanya biashara na kampuni za Marekani, kwa mujibu wa tovuti ya Wall Street Journal, Trump alisema.
Makampuni ya Marekani. yanaweza kuuza vifaa vyao kwa Huawei. Hapa tunasema vifaa ambavyo hivina tatizo kubwa kwenye usalama wa taifa. Nilisema hiyo ni Sawa., kwamba tutaendelea kuuza bidhaa hizo, hizi ni kampuni za Marekani ambazo hutengeneza bidhaa hizi. Nimekubaliana kuwaruhusu kuendelea kuuza bidhaa hizo ili kampuni za Marekani ziendelea.
Hata hivyo kupitia mkutano wa G20, Trump alisema kuwa China na marekani zitaendelea na mazungumzo ambayo pengine yanaweza kufanya kampuni ya Huawei kuondolewa kwenye list ya makampuni yasio ruhusiwa kuuza bidhaa nchini Marekani. Mazungumzo hayo yana tarajiwa kuanza rasmi mwezi julai tarehe mbili ambapo Raisi Trump atakutana tena na raisi wa China Xi Jinping.
Kwa sasa bado hakina uhakika kama kampuni ya Huawei itaendelea kutumia mfumo wa Android kwa asilimia 100 kama ilivyokuwa awali, ila kwa sababu makampuni ya marekani yameruhusiwa kufanya biashara na Huawei pengine pia Google itaendelea kuruhusu huawei kutumia mfumo wa Android kwenye simu zake kama kawaida.
Kwa sababu sakata zima hili limekaa kisiasa, pengine tuishie hapa kwa leo na tusubiri pale raisi wa marekani atakapo kutana na raisi wa china pengine kutakuwa na jipya la kiteknolojia la kukwambia, kujua zaidi kuhusu hili hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.