Tetesi : Kampuni ya Apple Kusitisha Programu Yake ya iTunes

Programu hiyo inasemekana kubadilishwa kabisa
Tetesi : Kampuni ya Apple Kusitisha Programu Yake ya iTunes Tetesi : Kampuni ya Apple Kusitisha Programu Yake ya iTunes

Kama wewe ni mtumiaji wa simu na vifaa vya Apple basi ni wazi kuwa unaijua programu ya iTunes, programu hii ndio yenye mkusanyiko wa vipindi vya sauti (podcast) kutoka kwa watu mbalimbali, Muziki na vipindi vya TV pamoja na Filamu.

Sasa kwa mujibu wa tovuti ya macrumors, kampuni ya Apple inatarajia kusitisha programu hiyo na badala yake kuja na apps tofauti za huduma mbalimbali, kwa mfano kwa upande wa filamu pamoja na TV, tayari Apple inayo huduma ya Apple TV Plus ambayo hii ni huduma kama ilivyo Netflix, hivyo ni wazi filamu zote na vipindi vya TV vitakuwa vinapatikana huko.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, tayari kampuni ya Apple imeshaanza kufuta vitu vilivyokwepo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya iTunes na kuacha kurasa hizo zenye wafuasi zaidi ya 1000 kuwa tupu kabisa bila post yoyote.

Tetesi : Kampuni ya Apple Kusitisha Programu Yake ya iTunes

Hata hivyo ripoti hizo zinadai kuwa, Apple inategemea kubadilisha pia link za iTunes kutoka link za itunes.apple.com kwenda kwenye link za kitu husika mtu anachotafuta, kwa mfano kwa muziki link zitabadilika na kuwa music.apple.com wakati kwenye apps itakuwa apps.apple.com.

Mabadiliko haya yanategemewa kutangazwa hapo siku ya kesho, Jumatatu ya tarehe 3 mwezi juni kwenye mkutano wa WWDC 2019 ambao unatarajiwa kuanza rasmi huko San Jose, nchini Marekani. Mbali na mabadiliko hayo, Apple pia inatarajia kutangaza ujio wa mifumo yake mipya ya iOS 13, macOS 10.15, watchOS 6 pamoja na tvOS 13.

Tanzania Tech tutakuwa mubashara kukujuza yote yatakayojiri kwenye mkutano huo hapo kesho, hivyo hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech bila kukosa. Kama unapenda habari kwa video unaweza ku-subscribe kwenye channel yetu na utaweza kupata habari mpya pamoja na kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use