Tecno Spark 3 Pro Simu ya Kwanza ya Tecno Kupata Android 10 Q

Simu hiyo ni miongoni mwa simu nyingine zaidi ya nane kutoka kwa washirika wa Google
Tecno Spark 3 Pro Simu ya Kwanza ya Tecno Kupata Android 10 Q Tecno Spark 3 Pro Simu ya Kwanza ya Tecno Kupata Android 10 Q

Kampuni ya Tecno imetajwa kwenye moja ya makampuni ambayo simu zake zitakuwa za kwanza kupata mfumo mpya wa Android 10 Q. Kupitia mkutano wa Google I/O 2019 kampuni hiyo imetajwa miongoni mwa makampuni mengine kumi na tatu ambayo simu zake zitapata mfumo huo za kwanza.

Tecno Spark 3 Pro Simu ya Kwanza ya Tecno Kupata Android 10 Q

Hata hivyo, kampuni ya Google imatangaza kuwa tayari simu mpya zaidi ya 10 kutoka kwa makampuni hayo 13 zimetangazwa kupata toleo la majaribio kuanzia siku ya jana. Simu hizo zilizotajwa ni pamoja na

Advertisement

Kwa sasa kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu moja kati ya hizo hapo juu basi unaweza kujaribu moja kwa moja mfumo mpya wa Android 10 Q ambao kwa sasa uko kwenye majaribio ya awamu ya tatu (Android Q beta 3). Ili kujaribu tembelea ukurasa HUU HAPA na simu yako kisha bofya sehemu ya View your eligible devices.

Hii ni mara ya kwanza kwa simu ya TECNO kuweza kutajwa na Google kama washirika kwenye kujaribu mfumo mpya wa Android, hatua hii ni nzuri sana kwa kampuni ya TECNO kwani  inaonyeshakuwa kampuni hiyo kwa sasa imekuwa na inaendelea kutambulika kwenye nchi mbalimbali tofauti na Afrika.

Kwa sasa kama unataka kujua zaidi kuhusu simu mpya za Tecno spark 3 na Spark 3 Pro, unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili pamoja na bei zake hapa nchini Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use