in

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48

Hizi hapa ndio sifa kamili pamoja na bei ya Motorola Moto Z4 kwa Tanzania

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48

Kampuni ya Motorola hapo jana imezindua ingizo jipya la simu za Moto Z, Simu ambazo kama unakumbuka vizuri kampuni ya Motorola ilizindua matoleo ya kwanza ya simu hizo hapo mwaka juzi 2017.

Sasa tofauti na matoleo hayo ya kwanza ya simu hizo, hapo siku ya jana Motorola imekuja na toleo la nne la simu hiyo ambayo ni Moto Z4. Motorola Moto Z4 inakuja na sifa nzuri sana huku macho yakiwa zaidi kwenye kamera yake ya Megapixel 48 pamoja na vifaa mbalimbali ambavyo hivi huitwa Moto Mods.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Ukiangalia simu hii kwa mbele inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD+ OLED, kioo ambacho pia kinakuja na uwezo wa resolution wa hadi pixel 1080 x 2340. Vilevile kioo hicho kinalindwa na ulinzi wa Corning Gorilla Glass 3, ulinzi ambao husaidia kioo hicho kisikwaruzwe kirahisi na vitu mbalimbali vyenye makali pale unapoweka simu hiyo mfukoni.

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48

Simu hii kwa mbele inakuja na kamera ya Megapixel 25 ambayo imewekwa kwenye ukingo wa mbele ambao unafahamika zaidi kama waterdrop notch. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera moja yenye uwezo wa Megapixel 48, kamera hiyo inauwezo wa kuchukua video za kawaida za 1080p pamoja na video za 4K.

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48

Mbali na hayo yote Moto Z4 inaendeshwa na processor ya Snapdragon 675 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 128. Simu hii pia inaendeshwa na battery ya 3500 mAh, yenye teknolojia ya Fast Charging. Sifa nyingine za Moto Z4 ni kama zifuatazo.

Sifa za Motorola Moto Z4

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya FHD+ OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz Kryo 460 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 460 Silver)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM675 Snapdragon 675 (11 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 612.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa memory card ya hadi TB 1.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25 yenye f/2.0, 0.9µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 48 yenye f/1.7, 1/2″, 0.8µm, PDAF, OIS ikiwa inasadiwa na Flash za LED dual-tone.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, BDS, GALILEO, SBAS. USB 3.1 ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Flash Grey na Frost White.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Motorola Moto Z4

Kwa mujibu wa motorola, Moto Z4 inategemewa kupatikana kuanzia tarehe 6 mwezi ujao na inategemewa kuja ikiwa na vifaa mbalimbali ambavyo vinaitwa moto mods huku bei ya simu hiyo ikiwa ni dollar za marekani $499, sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 1,148,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48

Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto Z4 Yenye Kamera ya MP 48
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.