Fahamu Hapa kwa Undani Sifa na Bei ya Huawei P Smart Z

Simu hii ni simu ya kwanza kutoka Huawei yenye kamera inayotumia Mota
Fahamu Hapa kwa Undani Sifa na Bei ya Huawei P Smart Z Fahamu Hapa kwa Undani Sifa na Bei ya Huawei P Smart Z

Kampuni ya Huawei hivi karibuni imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Huawei P smart Z, simu ya kwanza kutoka Huawei ambayo itakuwa na kamera ya mbele inayo endeshwa kwa kutumia mota.

Huawei P smart Z ni mwendelezo wa toleo la simu mpya ya Huawei P Smart ambayo ilitoka mapema mwaka huu (2019). Kwa upande wa sifa za Huawei P smart Z, kama nilivyo kwambia simu hii inakuja na kamera ya mbele ambayo inaendeshwa na mota huku kamera hiyo ikiwa na uwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.

Fahamu Hapa kwa Undani Sifa na Bei ya Huawei P Smart Z

Advertisement

Kioo cha simu hii kinakuja na ukubwa wa inch 6.59 huku kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya LTPS IPS LCD ambacho pia kina uwezo wa resolution hadi 1080 x 2340 pixels pamoja na uwiano wa 19.5:9.

Mbali na hayo simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma, kamera moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 5 zote zikiwa na teknolojia za HDR na panorama huku zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za hadi pixel 1080p@30.

Vilevile Huawei P Smart Z inaendeshwa na processor ya Hisilicon Kirin 710F ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 64, Hata hivyo ukubwa huo unaweza kuongezwa na memory card ya MicroSD card yenye uwezo wa hadi GB 512. Sifa nyingine za Huawei P Smart Z ni kama zifuatazo.

Fahamu Hapa kwa Undani Sifa na Bei ya Huawei P Smart Z

Sifa za Huawei P Smart Z

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.59 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2340 pixels (~391 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
  • Aina ya Processor – Hisilicon Kirin 710F (12 nm)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye f/2.0 pamoja na teknolojia ya HDR.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 (f/1.8, PDAF) na Kamera nyingine inayo Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Emerald Green, Midnight Black na Sapphire Blue.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Fingerprint (rear-mounted), accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Huawei P Smart Z

Kwa upande wa bei ya simu hii, inasemekana kwa mujibu wa Huawei bado haijajulikana rasmi ila inasemekana simu hii itakuwa ni ya gharama kidogo kuliko simu ile ya Huawei P Smart ambayo ilitangulia kutoka mapema mwaka huu 2019. Kujua bei ya simu hii pale itakapo toka rasmi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use