Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanahitaji kuwa na kompyuta ya bei rahisi kutokana na vifaa vya kununua kwa mafundi basi makala hii ni kwa ajili yako. Kupitia hapa utaweza kujifunza hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kuunganisha kompyuta kwa kutumia vifaa hivyo hadi hapo itakapo kuwa kompyuta inayofanya kazi.
Kitu cha msingi ni kuwa unahitaji kujua ni vitu gani unavyo hitaji kununua ikiwa pamoja na jinsi ya kuangalia ubora wa vitu hivyo. Kupitia hapa nitajitahidi kukupa ujuzi wa jinsi ya kupata vifaa hivyo lakini kitu cha muhimu kujua ni kuwa usiharakishe kununua vifaa hivi jipe muda wa kutosha ili uweze kupata vifaa bora zaidi.
TABLE OF CONTENTS
Mahitaji
Sasa ni muhimu sana kujua nini unachohitaji kwani bila kujua nini unacho hitaji huwezi kutengeneza kompyuta yako na pia unaweza kupoteza pesa na muda wako, kuwa makini na angalia list nzima ya vitu vyote na hakikisha unavipata vyote kabla ya kuanza hatua nzima.
- Motherboard – Hii inategemeana na uwezo wa motherboard lakini unaweza kupata kwa kuanzia Tsh 80,000 hadi 50,000.
- RAM – Hii pia inategemeana na aina ya motherboard lakini mara nyingi RAM za DDR2 ni bei nafuu kuliko zile za DDR 3. Unaweza kupata kwa Tsh 30,000 hadi 50,000 inategemeana na uwezo wa RAM.
- Hard Disk/SSD – Hii pia inategemeana na uwezo wa Motherboard hivyo kuwa makini sana unapo nunua Motherboard, unaweza kupata Hard Disk kwa Tsh 50,000 hadi 80,000 inategemeana na aina ya Hard Disk au SSD.
- Processor – Hii pia inategemeana SANA na aina ya Motherboard, ni vizuri kununua motherboard yenye processor ili kuweza kuepusha gharama nyingine za ziada. Lakini kama ukinunua inaweza kufika hadi Tsh 50,000 kutokana na uwezo wa Processor.
- Feni ya Processor – Hii pia ni vizuri kununua sambamba na Motherboard kwani feni zinatofautina hasa feni hizi za kupooza processor, kama ukinunua inaweza kufika Tsh 10,000 au zaidi. Hakikisha unapewa feni nzima na makava yake ya Plastiki.
- DVD Drive/CD ROM – Pia hii ni muhimu sana na ina tegemeana na aina ya Motherboard ila unaweza kupata kwa Tsh 20,000 hadi 30,000.
- Power Supply – Hii ni ya muhimu SANA na ni vizuri kuwa mwangalifu kwani hizi huwa na tabia ya kuharibika sana na ndio chanzo kikubwa cha kompyuta nyingi kuwepo kwa fundi, unaweza kupata kwa Tsh 50,000 hadi 70,000.
- Boksi la Kompyuta (Desktop) – Boksi hili kuwa linakuja la aina tofauti tofauti kutegemeana na Motherboard ni muhimu kwenye kununua box hili ukiwa na motherboard ili kuhakikisha motherboard yako ina fit vizuri kabisa, pia nunua misumari yote ya kufunga motherboard hiyo na sehemu nyingine. Unaweza kupata boksi kwa Tsh 50,000 hadi 80,000.
- Waya za Kompyuta – Kama umesha nunua vitu vyote sasa ni wakati wa kununua waya na hakikisha unapata kila waya ambayo inahitajika bila kusahau zile waya za hard disk ambazo ni vyema kununua na hard disk, waya zote unaweza kuzipata kwa Tsh 40,000 hadi 50,000.
Bajeti niliyofanya hapa ni kubwa sana na nimefanya hivi ili kuhakikisha unapata kila kitu chenye uhakika na ambacho kina uwezo mkubwa, lakini kwa ujumla unaweza kuwa na Tsh 200,000 hadi 250,000 na ukaunganisha kompyuta yako yenye nguvu sana.
Jinsi ya Kuunganisha Kompyuta (Desktop)
Basi baada ya kuangalia mahitaji sasa twende tukangalie hatua kwa hatua jinsi ambayo unaweza kuunganisha hadi kuweza kupata kompyuta inayoweza kufanya kazi kwa asilimia 100.
Hadi hapo nadhani utakuwa umeweza kuunganisha kompyuta yako, kama una maoni maswali au ushauri unaweza ktuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama umependa maujanja haya basu unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuchaji simu yako kwa kutumia malimao.
Nahitaji motherboard lakini contact yenu haionekani