Jinsi ya Kufufua Memory Card Iliyokufa ya Simu au Digital Kamera

Njia hii ni rahisi na haraka na inafanyakazi kwenye memory card za aina zote
Jinsi ya Kufufua Memory Card Iliyokufa ya Simu au Digital Kamera Jinsi ya Kufufua Memory Card Iliyokufa ya Simu au Digital Kamera

Ni wazi kuwa watu wengi sana bado wanatumia memory card kuhifadhi vitu mbalimbali vya muhimu, iwe unatumia memory card kwenye simu au hata kwenye kamera ya kidigitali ukweli unabaki pale pale kwamba, bado memory card ni sehemu muhimu ya vifaa vyetu vya kielektroniki.

Lakini tatizo linakuja, mara nyingi memory card hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi bila hata sababu ya msingi, yaani inakuwa kama vile memory card hiyo imeisha muda wake wa kufanya kazi yani inakufa tu bila hata wewe kutegemea.

Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamekutana na tatizo hili basi leo nimekuletea njia ambayo na uhakika ukitumia inaweza kusaidia kufufua memory card yako bila hata kupoteza chochote kilichopo ndani ya memory card hiyo.

Advertisement

Kitu cha msingi unachotakiwa kuzingatia ni kuwa na kompyuta ya Windows kwani hatua zote zinafanyika kupitia kompyuta. Basi kama unayo kompyuta yenye mfumo wa Windows basi endelea kwenye hatua zinazofuata.

Kwa kuanza chomeka memory card yako kwenye kompyuta, kisha baada ya hapo bofya kwenye sehemu ya kutafuta ya Windows kisha andika maneno CMD. Baada ya hapo Right Click kwenye sehemu ya Command prompt kisha chagua Run as administration.

Jinsi ya Kufufua Memory Card Iliyokufa ya Simu au Digital Kamera

Baada ya hapo programu ya command prompt itafunguka na endelea kwa kuandika maneno haya kwenye sehemu ya command, andika chkdsk / alafu andika herufi ya flash yako jinsi inavyo onekana kwenye computer yako kisha malizia kwa kuandika /f. Kwa mfano kama memory card yako inaonekana kwenye Windows ikiwa na herufi E basi itakuwa kama kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kufufua Memory Card Iliyokufa ya Simu au Digital Kamera

Baada ya kumaliza bofya Enter kwenye keyboard ya kompyuta yako, utaona programu hiyo ikianza kuangalia memory card yako na moja kwa moja utaona memory card yako imefanikiwa kupona. Kumbuka kama njia hii haito fanya kazi basi tuandikie kupitia maoni hapo chini tutakujuza njia nyingine ya kuweza kusaidia.

Kama unataka kujua njia ya kufufua flash iliyokufa unaweza kusoma hapa ili kujua njia ambazo zinaweza kusaidia kufufua flash yako kwa kutumia kompyuta.

Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani utaweza kujifunza maujanja haya yote kwa vitendo. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

18 comments
  1. Je nawezaje kufufua flash ambayo ukichomeka kwenye computer inaonesha kama ipo ila haionekan..

  2. Hi!
    Nimejaribu kufufua sd card yangu/memory card nimeshindwa,nimepata reply isemayo,”cannot open volume for direct access”. vp hapo mkuu,naomba maujanja hapa.

  3. nimejalibu hii njia imegoma kufanya kazi,
    nikichomeka memory kweny computer inaniomba kuformat nikiformat inafali

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use