Mara baada ya kampuni ya Google kutangaza kusitisha baadhi ya huduma zake kwa kampuni ya Huawei, kampuni nyingine za nchini Marekani zimejiunga kwenye list ya kampuni ambazo zimesitisha kufanya biashara na kampuni ya Huawei.
Kampuni hizo ni pamoja na kampuni ya InteI na Qualcomm, ambazo zote hizi zinajiusisha na utengenezaji wa chip kwa ajili ya vifaa mbalimbali vya kielektroniki. Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg, tofauti na kampuni ya Google ambayo imesitisha baadhi ya huduma zake, kampuni za intel na Qualcomm zenyewe zimetengaza kusitisha kufanya biashara na Huawei moja kwa moja hadi hapo itakapo tangazwa tena.
Kwa sasa kampuni ya Huawei hutumia zaidi Chip zake za Krin ambazo hizi hutengenezwa na kampuni ya Huawei na kutumika kwenye simu za Huawei pekee. Hata hivyo Huawei hutumia chip za makampuni hayo kwenye bidhaa zake kama vile laptop zake za Huawei Matebook.
Mbali na hayo, Huawei itoweza kutumia baadhi ya vifaa vingine kutoka kampuni hizo, kama vile Chip zinazotumika kutengeneza Modem na vifaa vingine vya mawasiliano ambavyo hutumiwa na kampuni ya Huawei kwenye baadhi ya bidhaa zake.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya wiki moja iliyopita kutoka tovuti ya Asia nikkei, Afisa mkuu wa Fedha wa Huawei alisema kuwa, kampuni ya Huawei haitokuwa na shida yoyote hata kama ikitokea baadhi ya kampuni za marekani kutouza Chip zake kwa kampuni ya Huawei.
Huawei ni kampuni inayo uza vifaa vya kielektroniki ambayo kwa mwaka 2018 ilifanikiwa kushika nafasi ya pili kwa uuzaji wa smartphone nyingi zaidi, na kuipiku kampuni ya Apple ambayo awali ndio ilikuwa ikishikilia namba mbili baada ya kampuni ya Samsung.
Mpaka sasa tayari kampuni ya Huawei imeshatoa tamko juu ya hatua hii inayoendelea ya baadhi ya kampuni za marekani kusitisha ushirikiano huo wa kibiashara unaotokana na agizo la serikali ya marekani kwa makampuni nchini humo,kulazimika kuwa na kibali maalum kutoka serikalini ili kufanya biashara na baadhi ya kampuni ya nchini China.
Update 20-05-2019 : Makala imeongezwa kuonyesha sehemu Huawei imetoa tamko rasmi