Huawei Yazuiwa Kutumia Memory Card za Micro SD na SD Card

Hii sio tatizo kwa Huawei kwani kampuni hiyo sasa inatengeneza memory card zake
Huawei Yazuiwa Kutumia Memory Card za Micro SD na SD Card Huawei Yazuiwa Kutumia Memory Card za Micro SD na SD Card

Bado katazo la kampuni ya Huawei kufanya biashara na kampuni za marekani linaendelea kuchukua sura mpya kwa kampuni ya Huawei. Hivi karibuni tuliona kampuni za Qualcomm na Intel zikisitisha kufanya biashara na kampuni ya Huawei, lakini kama haitoshi hivi karibuni kampuni ya Huawei imepigwa marufuku kutumia memory card za SD card na Micro SD.

Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5google, Huawei imeondolewa kwenye shirika lisilo la kibiashara la SD Association (SDA), shirika ambalo ndio uhusika kwenye kudhibiti na kutoa muongozo na viwango vya utumia wa Memory card za Micro SD na SD Card kwenye vifaa vya kielektroniki.

Huawei Yazuiwa Kutumia Memory Card za Micro SD na SD Card

Advertisement

Kutolewa huko kwenye shirika hilo kuna maana kuwa, Kampuni ya Huawei haitoruhusiwa kutumia memory card za Micro SD au SD Card kwenye vifaa vyake vya kielektroniki vinavyokuja, huku vifaa vingine vya kieletroniki kutoka Huawei ambayo tayari vipo sokoni vikiendelea kutumia sehemu hiyo kama kawaida.

Hata hivyo mabadiliko haya yanaweza yasi athiri sana ujio wa simu mpya kutoka Huawei, kwani kampuni hiyo tayari ilisha anza kutengeneza Memory card zake yenyewe ambazo zinaitwa (Nano Memory Card) ambazo hizi ni tofauti na memory card za Micro SD kwani zenyewe ni ndogo zaidi.

Huawei Yazuiwa Kutumia Memory Card za Micro SD na SD Card

Kwa sasa tayari Nano Memory card inatumika kwenye simu za Huawei P30 na P30 Pro ambazo tayari zipo sokoni tokea mwezi wa tatu mwaka huu 2019.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya wccftech, inasemekana kampuni ya Huawei ilijikusanyia shehena ya vifaa mbalimbali kutoka kampuni za marekani kabla ya katazo hilo, vifaa ambavyo vina uwezo wa kusaidia kampuni hiyo kuendelea kutengeneza simu zake kwa muda wa miezi sita, bila kuagiza vifaa vipya kutoka kampuni hizo za marekani.

Pamoja na hayo, lakini bado kampuni ya Huawei iko kwenye hali ngumu kwani vifaa hivyo havitaweza kutumika kutokana na katazo la kutumia vifaa hivyo kwenye simu mpya ambazo zinatoka baada ya tarehe ya katazo kutangazwa.

Kwa sasa ni wazi makatazo haya yanazuia kampuni ya Huawei kuendelea kutengeneza vifaa vipya, hivyo pengine tutegemee Huawei inaweza kuongea na marekani ili kuingia kwenye makubaliano ambayo pengine yanaweza kukomboa kampuni ya Huawei.

Kujua zaidi kuhusu sakata hili, hakikisha unaendelea kutembelea Tovuti ya Tanzania Tech kila siku tutakupa habari pindi tutakapo zipata rasmi.

3 comments
  1. Ninachokiona, haya makatazo yataiinua Huawei kuwa kampuni kubwa zaidi kiteknolojia. Wachina wataumiza vichwa usiku na mchana kuwa na vifaa vyao wenyewe.

  2. hapo huawei kama kaweza kuja memory cards zake ni shida lakini shida inakuja kama akaamua kuwashawishi wachina wanaotengeneza simu watumie vifaa vyake huoni wataziathiri kampuni za kimarekani zenye soko china

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use