Kampuni ya Samsung ni moja kati ya kampuni bora sana zinazo tengeneza TV za kisasa zinazoendana na wakati, Mwaka 2018 Samsung ilizindua TV ya 8K ambayo hiyo ndio ilikuwa ya kwanza kabisa kuwafikia wateja mbalimbali duniani kote kwani teknolojia ya 8K bado ni mpya sana kwa watumiaji wa TV pamoja na watengenezaji wa maudhui ya kwenye televisheni.
Lakini kama hiyo haitoshi hivi karibuni Samsung imetangaza aina mpya kabisa ya TV ambayo hii itakuwa na uwezo wa kusimama wima. Wote tunajua kuwa TV za sasa huja na muundo wa mlalo ambao hufanya picha kuweza kuonekana kwa urahisi zaidi na kwa upana, lakini kupitia TV hiyo mpya iliyopewa jina la The Sero ambayo maana yake ni wima, inakuja na uwezo wa kusimama wima na pia uwezo wa kuwa na muundo wa mlalo.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu TV hiyo mpya ya The Sero inauwezo wa kusimama wima huku picha na ikiwa na uwezo wa kugeuka ili kujaa kioo cha TV hiyo inapokuwa imesimama kwa mtindo huo. Lakini pia mbali ya kusimama wima TV hiyo pia inauwezo wa kuwekwa kwa muundo wa mlalo ambao ndio umezoeleka kwenye TV za hivi sasa.
TV hii inakuja kwa ukubwa wa inch 43 na inatumia panel iliyotengenezwa kwa teknolojia ya QLED yenye uwezo wa 60 watt. TV hii pia inakuja na spika za 4.1 channel speakers pia inakuja na mfumo wa Bixby pamoja na screen mirroring ambayo ina kusaidia kuunganisha simu yako na TV hiyo, hata hivyo kutokana na mtindo huo wa kusimama wima TV hii hufanya muonekano wa simu yako kuonekana vizuri zaidi kwani simu nazo zina muundo huo wa wima.
Kwa mujibu wa Samsung, The Sero au TV ya wima inasemekana kuanza kupatikana huko nchini Korea ya Kusini kuanzia mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu 2019 kwa Won Milioni 18.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 3,753,000 bila kodi.
Mbali na TV hiyo Samsung Pia imezindua TV nyingine ambazo zipo kama Fremu ambazo nazo zinategemewa kuanza kupatikana kipindi hicho.
Kwa sasa bado hakuna taarifa kama TV hizi zitapatikana nje ya Korea Kusini, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza pindi tutakapo pata taarifa kamili za ujio wa simu hizi hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla.