in

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Tovuti hizi ni rahisi kutumia na utaweza kutengeneza app nzuri za kisasa

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Ni wazi kuwa Android ni moja ya mfumo maarufu sana hivi sasa, mwaka 2017 mfumo huu ulishikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa mfumo unaotumiwa zaidi duniani, huku soko la Play Store kwa kipindi hicho likiwa na idadi ya Apps zaidi ya milioni 3.5 hapo mwezi wa desemba mwaka juzi (2017).

Sasa kutokana na umaharufu wa mfumo huu ni wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakitaka kutengeneza Android apps kuliko hata app za mifumo mingine, sasa kama wewe ni mmoja wa watu waliokuwa wanataka kutengeneza Android app kwa ajili ya tovuti yako basi makala hii ni kwa ajili yako.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia tovuti mbalimbali ambazo zitakusaidia kutengeneza App kupitia tovuti hizo bila kuwa na ujuzi wowote na bila kutumia gharama yoyote. Kumbuka tu baadhi ya tovuti hizi zinahitaji malipo ili kutoa baadhi ya huduma ila unaweza kutengeneza apps bila hata kuwa na huduma hizo, basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja tukangalie tovuti hizi.

AppYet

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Appyet ni moja ya tovuti bora na rahisi kutumia kutengeneza App za Android, tovuti hii inakuruhusu kutengenza app kwa ajili ya blogger au kwa kutumia tovuti yoyote yenye kutumia RSS Feed. Apps nyingi za hapa Tanzania zimetengenezwa kwa kutumia tovuti hii hivyo unaweza na wewe kutembelea tovuti hii ili kujaribu kutengeneza app yako, kitu cha msingi unachotakiwa kuwa nacho ni barua pepe ambapo app hiyo hutumwa baada ya kutengenezwa.

Jaribu Apps Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android (2020)

Tembelea Appyet Hapa

Andromo

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Kama wewe ni somaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi tovuti hii sio ngeni kwako, Andromo ni tovuti ambayo tayari tulisha weza kuonyesha jinsi ya kutumia na kutengeneza app za Android kwa urahisi, kama unataka kujua jinsi ya kutumia basi unaweza kusoma makala nzima hapa. Mbali na hayo Andromo haina tofauti sana na tovuti iliyopita kwani unahitaji kuwa na barua pepe ili kupokea app pale inapo malizika kutengenezwa.

Tembelea Andromo Hapa

Appsbar

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Appbar ni tovuti nyingine nzuri ya kukusaidia kutengeneza apps za Android pamoja na iOS bila kuwa na ujuzi wowote, tovuti hii ni nzuri sana na inaweza kukusaidia kutengeneza app kwa haraka na rahisi. Kama ilivyo tovuti zingine kwenye list hii pia unahitaji kuwa na email ili kuweza kutumia tovuti hii kwa urahisi na haraka.

Tembelea Appbar Hapa

Appypie

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Appypie ni tovuti nyingine ambayo nahisi watu wengi watakuwa wanafahamu, tovuti hii ni bora sana kwa sababu inakupa uwezo wa kutengeneza app nzuri sana. Tofauti ya tovuti hii na nyingine kwa list hii ni kuwa appypie inatengeneza apps ambazo zinakuja na matangazo ambayo ili kuondoa matangazo hayo ni lazima kulipia kiasi kidogo. Andromo pia inakuja na sehemu kama hii.

Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja (Android)

Tembelea Appypie Hapa

Appsgeyser

Tovuti za Kusaidia Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi

Appsgeyser ni tovuti nyingine bora sana ya kutengeneza apps za Android, tovuti hii ni nzuri sana kwa sababu inakusaidia kutengeneza apps ambazo unaweza kuweka matangazo na kupata pesa kutokana na app yako. Tovuti hii ni rahisi sana kutuia na ukweli inafanya kazi vizuri sana, ili kutumia tovuti hii unahitaji barua pepe ili kuweza kutumia kwa urahisi na haraka.

Tembelea Appsgeyser Hapa

Na hizo ndio baadhi tu ya tovuti ambazo unaweza kutumia kutengeneza Apps za Android, kumbuka unaweza kutengeneza app kwa kutumia tovuti hizo bure kabisa na pia kuna baadhi ya tovuti hapa ambazo unaweza kulipia ili kupata sehemu nyingi zaidi kwenye app yako, lakini pia unaweza kuchagua kutumia tovuti hizi bure kabisa.

Kwa habari zaidi na makala nyingine kama hizi hakikisha una tembelea Tanzania Tech tutakujulisha zaidi pale tutakapokuwa na list mpya kama hii.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.