Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom

Zifahamu hapa kwa undani sifa na bei ya Oppo Reno na Oppo Reno 10X Zoom
Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom

Kampuni ya Oppo hivi leo imezindua simu yake mpya ya Oppo Reno, simu ambayo inakuja ikiwa ndio simu ya kwanza kabisa kutoka chini ya brand mpya ya Oppo ambayo inaitwa Reno. Siku za karibuni kampuni hiyo ili tangaza kusajili brand hiyo mpya ya simu ambayo simu ya kwanza ndio imetangazwa rasmi siku ya leo huko nchini China.

Oppo Reno inakuja kwa matoleo mawili Oppo Reno 10X zoom na Oppo Reno ya kawaida, Simu zote zinakuja kwa muundo unaofanana lakini kuna baadhi ya sifa simu hizi zina tofautiana.

Advertisement

Sifa za Oppo Reno

Oppo Reno ya kawaida inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2340 pixels. Kioo hicho hakina sehemu ya kamera ya mbele kwani kamera ya mbele ya simu hii inafanana sana na simu nyingine ya Oppo Find X ambayo yenyewe pia huslide kwa nyuma pale mtu anapotaka kutumia kamera ya mbele.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom

Kwa upande wa Oppo Reno inakuja na aina mpya ya kamera kwani kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu kamera hiyo inatoka kwa upande na sio kama ku-slide kama ilivyo Oppo Find X.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom

Kamera hiyo ya mbele inakuja na uwezo wa Megapixel 16 huku ikiwa na uwezo wa kurekodi video hadi za 1080p@30, Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili kamera moja ikiwa na Megapixel 48 na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote za nyuma zinasaidiwa na flash ya Dual LED Flash pamoja na HDR na panorama. Sifa nyingine za Oppo Reno ni kama zifuatazo.

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye ColorOS 6
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (10 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
  • Ukubwa wa Ndani (ROM) – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine GB 256 huku zote zikiwa na hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM GB 6 na nyingine GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 inayotumia Mota maalum.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye ff/1.7, 1/2.0″, 0.8µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, depth sensor. Kamera zote zikiwa zinasadiwa na dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3765 mAh yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, GALILEO, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa nne za Fog Sea Green, Extreme Night Black, Nebula Purple, Pink Mist.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Oppo Reno

Kwa upande wa bei ya Oppo Reno simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku za karibu huku bei yaki ikianzia Yuan 2,999 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,034,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ROM wa GB 128. Kwa upande wa Reno yenye RAM GB 6 na Rom GB 256 itauzwa kwa Yuan 3,299 ambayo ni sawa na Tsh 1,138,000 bila kodi. Toleo lenye GB 8 za RAM na GB 256 za ROM litauzwa kwa Yuan 3,599 ambayo ni sawa na Tsh 1,241,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Sifa za Oppo Reno 10x Zoom

Kwa upande wa Oppo Reno 10x Zoom, kama nilivyo kwambia simu hizi hazitofautiani sana kwa muonekano bali kwenye simu hii kamera, battery pamoja na processor ndio vitu vikubwa vya tofauti. Kamera ya Oppo Reno 10x Zoom inakuja na teknolojia ya ku-zoom hadi mara kumi zaidi, pia simu hii inakuja na kamera tatu za nyuma badala ya mbili kama ilivyo Oppo Reno.

Oppo Yazindua Simu Mpya za Oppo Reno na Reno 10X Zoom

Kamera hizo za nyuma zinakuja na uwezo wa Megapixel 48, Megapixel 13 pamoja na Megapixel 8 huku kamera zote zikisaidiwa na teknolojia ya HDR na panorama. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera zinazo fanana na Oppo Reno.

Kwa upande wa processor simu hii inakuja na processor ya Qualcomm Snapdragon 855 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6 au GB 8. Battery ya simu hii ni kubwa kidogo kuliko ile ya Oppo Reno ya kawaida kwani yenye inakuja na uwezo wa 4065 mAh battery, Sifa nyingine za Oppo Reno 10x Zoom ni kama zifuatazo.

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.6 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye ColorOS 6
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani (ROM) – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine GB 256 huku zote zikiwa na hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM GB 6 na nyingine GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 inayotumia Mota maalum.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye ff/1.7, 1/2.0″, 0.8µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye Periscope, f/3.0, (telephoto), 5x optical zoom, OIS, Laser/PDAF. Kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 8 yanye, f/2.2, 13mm (ultrawide). Kamera zote zinasadiwa na dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4065 mAh yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, GALILEO, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa nne za Fog Sea Green, Extreme Night Black, Nebula Purple, Pink Mist.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Oppo Reno 10x Zoom

Kwa mujibu wa The Verge Oppo Reno 10x Zoom inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao huku bei yake ikianzia Yuan 3,999 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,379,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ROM wa GB 128. Kwa upande wa Reno yenye RAM GB 6 na Rom GB 256 itauzwa kwa Yuan 4,499 ambayo ni sawa na Tsh 1,551,000 bila kodi. Toleo lenye GB 8 za RAM na GB 256 za ROM litauzwa kwa Yuan 4,799 ambayo ni sawa na Tsh 1,655,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

2 comments
  1. Hapo kwenye selfie camera umesema inatumia moto maalumu. Unamaanisha kuwa selfie camera ina moto wake tofauti na wa betri la simu au maana yake nini?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use