Wakati tukiwa bado tunasubiri simu ya kwanza ya Tecno yenye kamera tatu kwa nyuma, kampuni ya Infinix hapo jana imekuwa ya kwanza kuzindua simu mpya za Infinix Hot S4 na Hot S4 Pro ambazo zinakuja na kamera tatu kwa nyuma.
Mbali na kamera hizo, Hot S4 inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Kioo hicho kwa mbele kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama waterdrop notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele yenye Megapixel 32.
Infinix Hot S4 inakuja na kamera tatu ambazo hizi zina uwezo wa Megapixel 13, Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, kamera zote za nyuma zinasaidia na flash ya Quad-LED flash na teknolojia ya AI ambayo inasaidia kufanya picha ziwe na muonekano mzuri.
Kwa upande wa processor, simu hizi zinaendeshwa na processor ya Mediatek’s Helio P22 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 kwa infinix Hot S4 na GB 6 kwa Infinix Hot S4 Pro, matoleo hayo pia yanatofautiana kwenye ukubwa wa ROM kwani Hot S4 inakuja na ROM ya GB 32 na Hot S4 Pro inakuja na ROM ya GB 64. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi GB 128. Sifa nyingine za Infinix Hot S4 na Hot S4 Pro ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Infinix Hot S4
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.22 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa OSX V5.0
- Uwezo wa Processor – Quad-core CPU 4×2.2, GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek’s Helio P22 SoC
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili Hot S4 ina Ukubwa wa GB 32 na Hot S4 Pro ina ukubwa wa ndani wa GB 64, simu zote mbili zinakuja zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili, Infinix Hot S4 inakuja na RAM ya GB 3 na Hot S4 Pro inakuja na RAM ya GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye nyingine ikiwa na Megapixel 8 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Quad-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Milan Black, Sapphire Cyan na Gold.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Infinix Hot S4
Kwa upande wa bei Infinix Hot S4 inatarajiwa kuingia sokoni nchini Nigeria hivi karibuni na inasemekana kuuzwa kwa Naira NGN 49,900 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 322,000 kwa toleo la Infinix Hot S4. Kwa upande wa Infinix Hot S4 Pro inategemea kuuza kwa Naira NGN 64,500 ambayo ni sawa na Tsh 416,000. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa Tanzania.
Hiii simu nasubiri sana kwa hamu
Aisee wakuu ikitoka mnishtue
Maoni*tunashukuru bei ni moja kwa mikoa yote tanzania?au kuna mikoa iko chini kidogo?
Pesa mtandaoni
Nimenunua hii infinix s4 inanionyesha storage GB 32 lakin nimeweka picha tu imejaa naomba nipatiwe msaada
Kwangu mm nafurahia sana kununua infinix S4 sema tyu inagandaganda kidogo