Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A60

Zifahamu hapa sifa kamili na bei ya Samsung Galaxy A60
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A60 Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A60

Baada ya tetesi za ujio wa simu mpya ya Galaxy A60, hatimaye hivi leo kampuni ya Samsung imezindua rasmi simu hiyo huko nchini China. Kama ilivyo semekana kwenye tetesi Galaxy A60 inakuja na teknolojia ya kisasa pamoja na uwezo mkubwa wa kamera.

Simu hii inakuja na kamera tatu kwa nyuma huku kamera moja ikiwa na Megapixel 32, kamera nyingine ikiwa na megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na megapixel 5. Mbali na hayo kwa mbele simu hii inakuja na kamera kubwa yenye Megapixel 32 ambayo ipo juu ya kioo kama ilivyo kamera za Galaxy S10.

Advertisement

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A60

Mbali na hayo Galaxy A60 inakuja na kioo cha inch 6.3 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, kioo ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2340 pixels. Vilevile kioo cha Galaxy A60 kinakuja na teknolojia mpya ambayo inafanya kioo hicho kutumika kutoa sauti badala ya spika za loudspeaker ambazo huwa kawaida ndio zinatoa sauti ya muziki na ringtone kwenye simu.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A60

Simu hii haina sehemu ya Spika kwa sababu kioo hicho ndicho kinachotumika kama spika kama ilivyo simu mpya ya LG G8 ThinQ. Mbali na hayo Galaxy A60 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 675 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa memory card hadi GB 512. Sifa nyingine za Galaxy A60 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A60

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.3 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~409 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz Kryo 460 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 460 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM675 Snapdragon 675 (11 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 612.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 32 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Gold.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A60

Kwa upande wa bei Galaxy A60 inasemekana kuja ikiwa inauzwa kwa Yuan ya China CNY 1,999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 692,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha Fedha.

Nini maoni yako unaonaje simu hii mpya ya Samsung Galaxy A60, Je unadhani ni simu bora ambayo ungependa kuwanayo kwa mwaka huu 2019..? Tuambie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use