Hivi karibuni kampuni ya Samsung ilitoa simu yake ya kwanza inayojikunja baada ya majaribio ya muda mrefu, Galaxy Fold ilitangazwa sambamba na simu za Galaxy S10 hapo mwezi February mwaka huu 2019 huku simu hizi zikitegemewa kupatikana baadae mwaka huu.
Miezi miwili badae kampuni ya Samsung tayari imeanza kuchukua oda za kusambaza simu hizi huku bei yake ikiwa takribani zaidi ya milioni 4,000,000 za kitanzania, lakini kabla wateja mbalimbali kuanza kupata simu hizi baadhi ya waandishi wa habari hupata nafasi ya kupokea simu hizi mapema kwa ajili ya kufanya mapito (Review) na kutoa maoni yao.
Sasa katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya simu ambazo walipewa waandishi kwa ajili ya kufanya mapitio (Review) zimekubwa na matatizo yanayo fanana. Tatizo la kwanza limeripotiwa hapo jana na waandishi wa tovuti za CNBC na The Verge ambapo kupitia kurasa zao za Twitter waliandika kuwa simu hizi zimeharibika baada ya matumizi ya siku mbili tu toka kuzipokea.
https://twitter.com/stevekovach/status/1118571414934753280
Tatizo kubwa ambalo limeonekana kuripotiwa hadi sasa ni tatizo la kioo ambacho kina onekana kutokuwa imara na kuharibika pale watumiaji wanapo bandua stika ya plastiki ambayo inakuwa juu ya kioo hicho kama screen protector. Hata hivyo baadhi ya waandishi wanadai kuwa stika hiyo haijawekewa maelezo yoyote na ni rahisi mtu kubandua kwa kudhani ni platiki ya kulinda kioo au (screen protector).
The phone comes with this protective layer/film. Samsung says you are not supposed to remove it. I removed it, not knowing you’re not supposed to (consumers won’t know either). It appeared removable in the left corner, so I took it off. I believe this contributed to the problem. pic.twitter.com/fU646D2zpY
— Mark Gurman (@markgurman) April 17, 2019
— Khalifa Al Haroon – Mr. Q (@iloveqatar) April 17, 2019
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, madhara yanayotokana na kubandua stika hiyo ni makubwa na yanaweza kusababisha kioo cha simu hiyo kuharibika kabisa na kuacha kufanya kazi. Hata hivyo inasemekana maelezo ya onyo juu ya kubandua stika hiyo hayapatikani kwa urahisi hivyo kupelekea watu kutojua kuhusu umuhimu wa stika hiyo.
Mbali na matatizo ya Stika hiyo matatizo mengine ambayo yameweza kuonekana na waandishi hao ni pamoja na matatizo ya kioo ambayo yalitokea japo kuwa waandishi hao hawakutoa stika hizo kwenye kioo hicho, hata hivyo matatizo hayo kwa upande wao yalikuwa tofauti kwani Galaxy Fold ilionekana kuacha kufanya kazi upande mmoja wa simu hiyo huku upande mwingine ukifanya kazi kama kawaida.
https://twitter.com/stevekovach/status/1118573410785820672
Kupitia maelezo yaliyotolewa na kampuni ya Samsung baada ya kupata malalamiko hayo, Samsung imesema kuwa matatizo yaliyotokea kwa baadhi ya waandishi ambao hawaku bandua stika kwenye vioo vya simu zao yatafanyiwa uchunguzi na kutolewa ufafanuzi hapo baadae. Samsung pia imesema itaweka maelezo zaidi ya kuwajulisha wateja kutobandua stika hiyo kwenye vioo vya Galaxy Fold na kukubali kuwa inawezekana maelezo hayo yalikuwa hayapatikani kwa urahisi.
Galaxy Fold ni simu ambayo ni wazi kuwa inahitaji kumilikiwa na watu ambao watakuwa wastarabu sana na pengine simu hii inaweza isifae kwa kila mtu kutokana na muundo wake. Vilevile kama unavyoweza kuona hapo chini Galaxy Fold inakuja na sumaku zenye nguvu sana kiasi cha kuweza kunasa kwenye baadhi ya vitu ambavyo wakati mwingine vinaweza kuwa mfukoni pamoja na simu hiyo.
Sasa nadhani utakuwa umejipanga wakati unataka kununua simu hii, kujua zaidi kuhusu sifa na muonekano wa Galaxy Fold unaweza kusoma zaidi hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.