Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Pamoja na App ya Android Bure

Tengeneza Website pamoja na app yake bure bila kulipia
Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Pamoja na App ya Android Bure Jinsi ya Kutengeneza Tovuti Pamoja na App ya Android Bure

Habari Guys na karibuni kwenye maujanja, siku tatu zilizopita kuna baadhi ya watu waliandika barua pepe wakitaka kujua jinsi ya kutengeneza tovuti au website pamoja na application bila kulipia. Ukweli ni kwamba zipo njia za kufanya hivi na zinaweza kukusaidia kutengeneza tovuti ya bure pamoja na app yake kwa muda mfupi.

Basi kutokana na swali hilo nimeona nirudie baadhi ya njia ambazo tayari zipo hapa Tanzania tech lakini sasa nimeona niunganishe njia hizi kwa pamoja ili kuleta urahisi kwa msomaji wa makala hii. Lakini kama ulikuwa unataka kujifunza jinsi ya kutengeneza website pekee yenye muonekano wa kisasa basi unaweza kusoma makala hapa itakuelekeza kwa kina.

Advertisement

Vilevile kama unataka kujifunza kutengeneza App pekee, basi unaweza kusoma makala hapa jinsi ya kutengeneza app ya Android kwa kutumia simu yako na bila kulipia kwa namna yoyote. Njia zote hizi ndio ambazo zipo kwenye makala hii lakini sasa zitakuwa pamoja ili kuleta urahisi zaidi kwako, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

Jinsi ya Kutengeneza Tovuti

Sasa labda tuongelee mahitaji machache unayo hitaji kabla ya kutengeneza tovuti hii ya bure. Kwanza unahitaji akaunti ya Google ambayo najua wote tunayo, pili unahitaji internet ambayo pia najua unayo sasa kama unavyo vitu vyote hivi sasa unaweza kuanza hatua hizo hapo chini.

Baada ya kumaliza kuangalia Video hiyo hapo juu natumaini umeweza kutengeneza Tovuti bora ya bure kabisa bila kutumia garama yoyote. Kama unataka kuangalia website ambayo nilitengeneza kupitia njia hii unaweza kuangalia hapa, pia kama unataka Template nzuri kwaajili ya tovuti yako basi unaweza kuzipata hapa, bila kusahau tovuti ya freenom kwaajili ya domain yako ya bure inapatikana hapa. Basi baada ya kuangalia jinsi ya kutengeneza tovuti twende tukangalia jinsi ya kutengeneza app kwa ajili ya tovuti yako.

Jinsi ya Kutengeneza App ya Android

Kwa upande wa mahitaji ili uweze kutengeneza app unahitaji internet ambayo najua unayo na pia unahitaji barua pepe yenye kufanya kazi, pia unahitajika kuandaa picha kwaajili ya app yako picha zinazo hitajika ni kama Icon picha moja pana yenye upanda wa 800 na urefu wa 400, kama unavyo vyote hivyo basi utakuwa uko tayari kujifunza hatua ya pili ya kutengeneza App kwaajili ya tovuti yako uliyo tengeneza app juu.

Maelezo mengine ya muhimu kuhusu njia hii ni kuwa unahitaji kuingia kweye tovuti ya Andromo hapa, kisha wakati wa kutengeneza app unaweza kufuata maelezo hayo hapo chini ili kujua nini kinawekwa wapi.

  • About – Hapa utaweka ukurasa wa kuhusu programu yako au wewe
  • Audio Player – Hapa utaweza kuweka sehemu ya kucheza muziki
  • Contact – Hapa utaweza kuweka anwani yako
  • Custom Page – Hapa utaweza kuweka ukurasa wowote unaotaka
  • Email – Hapa utaweza kuweka barua pepe
  • Facebook – Hapa utaweza kuweka ukurasa wa facebook
  • Flickr – Hapa utaweza kuonyesha picha kutoka mtandao wa Flick
  • Google Play – Hapa utawea kuonyesha link kwenda kwenye Google Play
  • HTML Archive – Hapa utaweza kuweka ukurasa unaotumia HTML
  • Map – Hapa utaweza kuweka ramani
  • PDF – Hapa utaweza kuweka file la PDF
  • Phone – Hapa utaweza kuweka namba ya simu
  • Photo Gallery – Hapa utaweza kuweka picha mbalimbali
  • Podcast – Hapa utaweza kuweka mfumo wa Podcast
  • RSS Feed – Hapa utaweza kuweka RSS fee ya blog yako
  • SHOUTcast Radio – Hapa utaweza kuweka radio kwenye app yako
  • Twitter – Hapa utaweka ukurasa wao wa Twitter
  • Website – Hapa utaweka tovuti yako
  • YouTube – Hapa utaweka ukurasa wako wa Youtube

Kwa kufuata njia zote hizo hapo juu utakuwa umeweza kutengeneza app kwaajili ya tovuti yako na pia ambayo ulitengeneza awali. Kama unataka kuona app ambayo nilitengeneza kwa kutumia njia hii unaweza kudownload app hiyo hapa.

Kama kuna mahali utakuwa umekwama basi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi kama haya unaweza kutembelea kipengele cha maujanja au hakikisha una jiunga na channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

7 comments
  1. Somo zuri
    Naomba nitoke nje ya mada kidogo ni ulize hivi simu ambazo ziko rooted kuna uwezekano wa ku unroot?

  2. Habari ya kazi mkuu, samahani Mimi nina swali lakini nje ya mada hii, nina simu yangu aina ya huawei g 730 inawaka na kuzima na imfrashiwa lakini tatizo lipo palepale je waweza kunisaidia juu ya tatizo hilo?

  3. Naomba unijuze zaidi maana mimi naamini kama umeamua kutoa darasa hapa basi unania njema na watanzania wenzako nami ni miongoni mwa watanzania wanaotaka kujifunza zaidi hebu nibeep mimi nitapiga kwasababu mimi ndo mwenye shida 0785440209 au 0719975551 0767975551

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use