Ni kweli kwamba mara nyingi wengi wetu tunakuwa na smartphone zetu kila mahali tunapo kwenda, kwa sababu hii ni wazi kuwa tunaweza kutumia simu hizi pia kuweza kutusaidia kwenye mambo mbalimbali ya kiafya, ndio maana kwenye makala hii nimekuletea apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kulinda afya yako kupitia simu yako ya Android.
Apps hizi ni nzuri sana kwa sababu zinakusaidia kuendelea kulinda afya yako huku unatumia simu yako kama kawaida, basi bila kupoteza muda twende tukaangalie app hizi nzuri.
Night owl ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kulinda macho yako hasa wakati wa usiku, app hii ni nzuri kwa sababu inakupa uwezo wa kupunguza mwanga ambao huumiza macho unapotumia simu kwenye giza au mwanga hafifu. Kupitia app hii utaweza kupunguza mwanga huo na utaweza kulinda macho yako hasa wakati wa usiku.
Kama wewe umekuwa unajisahau kufanya mambo ya msingi unapotumia smartphone basi app hii ni nzuri sana kwako, Water Drink Reminder ni app nzuri ambayo inakusaidia sana kuweza kukumbuka muda wa kunywa maji. Sidhani kama hapa nina haja ya kuweza kukwambia umuhimu wa kunywa maji.
Sleep time ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya afya yako, app hii inakusaidia sana kuweza kugundua jinsi unavyolala usiku kwani inaweza kukupa data za muhimu pale unapokuwa umelala hasa wakati wa usiku. Unachoatakiwa kufanya ni kudownload app hii kisha weka simu yako chini ya mto na moja kwa moja app hii itaweza kukwambia ni kwa namna gani unalala, iwe unakoroma usiku au una angaika sana usiku app hii itakupa data zote.
Kama unatumia simu ya Samsung basi lazima unajua app hii kwani inakuja moja kwa moja kwenye simu za Samsung, App hii ni nzuri kwani inakusaidia kukupa taarifa za mazoezi madogo madogo hasa ya kutembea. Samsung Health inakupa uwezo wa kujua hatua ngapi umetembea pale unapo tembea pia inakupa taarifa hatua ngapi unahitaji kutembea kwa siku ili kuupa mwili nguvu na afya inayotakiwa.
Kama unataka kupunguza mwili huku unatumia simu yako basi app hii ya Pedometer ni app nzuri sana kwako, App hii ni kama app ya Samsung Health lakini app hii ni nzuri zaidi kwani inafanya zaidi ya kuhesabu hatua. App hii inakupa uwezo wa kukupa muelekezo nini ufanye ili kupunguza uzito kwa haraka.
Kama kwa namna yoyote wewe ni mwanamke na umechoshwa na kuwa na tumbo kubwa basi app hii itakusaidia sana, Lose Belly Fat at Home ni app nzuri kwa sababu itakupa mazoezi ya kawaida ya mwili ambayo yatasaidia sana kuweza kupunguza kitambi kwa wanawake.
App ya mwisho kwenye list hii ni app ya Habit Formation, app hii itakusaidia kuweza kubadilisha afya yako ndani ya siku 21. App ni nzuri sana kwa sababu inakusaidia kuweza kukumbuka muda wa kunywa maji, muda wa kufanya mazoezi ya kawaida ya mwili pamoja na muda wa kufanya mambo mbalimbali ambayo yatasaidia sana afya yako. Ni ukweli kama ukifuata hatua zote ndani ya siku 21 utaweza kuona mabadiliko kwenye afya yako.
Na hizo ndio apps nzuri nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kumbuka unaweza kupakua app zote hizi kupitia soko la Play Store kwa kubofya link husika. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kuunganisha simu moja na nyingine unaweza kusoma hapa, na uhakika utaweza kufurahia app hizo.