Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Zifahamu hizi hapa ndio simu mpya za Huawei P30 na Huawei P30 Pro
Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Wakati kampuni ya Samsung tayari imeshazindua simu zake za Flagship ambazo ni Samsung Galaxy S10 na S10 Plus, kampuni ya Huawei yenyewe ndio inamalizia kujiandaa na uzinduzi wa simu zake za Flagship ambazo ni Huawei P30 na Huawei P30 Pro.

Sasa kabla ya simu hizi kuzinduliwa rasmi mwezi huu tarehe 26, tayari muonekano sifa pamoja na bei za simu hizi mpya zimeshavuja kabla ya tarehe hiyo kufika. Kupitia tovuti mbalimbali, Huawei P30 imekuwa ikionekana kwa muda mrefu sana kuanzia mwezi huu, na simu ya Huawei P30 Pro muonekano wake ndio umevuja hivi karibuni.

Advertisement

Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Kama unavyo weza kuona, upande wa kushoto ni simu mpya ya Huawei P30 na upande wa kulia ni Huawei P30 Pro. Kama inavyo onekana simu hizi zinatarajia kuja na kamera tatu kwa nyuma kwa Huawei P30 na kamera nne kwa nyuma kwa Huawei P30 Pro.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, P30 inakuja na kamera za Megapixel 40, 16, na Megapixel 8. Kamera hizo zinauwezo wa kuchukua video za 4K huku zikiwa na teknolojia ya Leica optics, mbali na hayo kamera ya mbele ya simu hii inategemewa kuja na uwezo mkubwa wa hadi Megapixel 32.

Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Kwa upande wa P30 Pro, yenyewe inakuja kamera za Megapixel 40, 20, 8 na kamera nyingine ni TOF 3D camera ambayo hii inafanya picha ziwe na mwanga zaidi. Vilevile pia Huawei P30 Pro inakuja na uwezo wa kuchukua video za 4K huku ikiwa na teknolojia ya Leica optics. Kwa upande wa kamera ya mbele simu hizi zote zinafanana kwa kujua na kamera za MP 32.

Simu za Huawei P30 na P30 Pro Zavuja Kabla ya Kuzinduliwa

Kwa upande mwingine simu hizi zinakuja na sifa tofauti kidogo, kwa mfano Huawei P30 Pro inakuja kwa matoleo matatu yenye ukubwa wa ROM tofauti kama vile GB 128, GB 256 au GB 512 zote zikiwa zinasaidiwa na RAM ya GB 8. Huawei P30 yenyewe inakuja na toleo moja tu ambalo litakuwa na ukubwa wa ROM wa GB 128 na RAM ya GB 6.

Kingine cha muhimu kujua ni kuwa, simu hizi zote zitakuja na teknolojia za kuzuia maji na vumbi pamoja na processor za kisasa kutoka Huawei zinazo julikana kama HiSilicon Kirin 980. Pia simu hizi zitakuja na uwezo wa kuongezewa ukubwa wa ROM kwa kutumia Memory Card, lakini itakuwa sio memory card zile za MicroSD bali itakuwa ni NM Card ambazo hizi ni ndogo kuliko zile memory card za kawaida.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, inasemekana simu hizi zitaingia sokoni rasmi mwezi wa nne mwaka huu 2019. Kwa habari zaidi pamoja na sifa kamili na bei ya simu hizi hakikisha una ungana nasi kila siku kupata habari za simu hizi pamoja na habari nyingine za teknolojia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use