Kampuni ya Samsung hivi leo imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Galaxy A70, Simu hii inakuja na sifa nzuri sana ambazo hata simu ya Samsung Galaxy S10 na S10 Plus hazina. Hata hivyo simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kabisa mwezi wa nne mwaka huu 2019.
Pamoja na kuwa simu hiyo itazinduliwa rasmi mwezi wa nne, lakini tumefanikiwa kupata muonekano pamoja na baadhi ya sifa za simu hii mpya kutoka Samsung.
Kwa kuanza, Galaxy A70 inakuja na kioo cha inch 6.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED. Kwa juu simu hii inakuja na ukingo wa juu ambao umepewa jina la Infinity-U display, kwenye ukingo huo kuna sehemu ya kamera ya mbele ambayo hii inakuja na uwezo wa Megapixel 32. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu za Megapixel 32, 8 pamoja na Megapixel 5.
Kwa mujibu wa tovuti ya XDA developer, processor ya simu hii bado haijajulikana rasmi ila inasemekana simu hii inaendeshwa na processor ya Octa Core ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 8 au GB 6, pamoja na ukubwa wa ROM kati ya GB 64 na GB 128. Pia Galaxy A70 inakuja na sehemu ya memory card hivyo unaweza kuongeza ukubwa wa ROM kwa Micro SD card hadi ya GB 512. Sifa nyingine za Galaxy A70 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Samsung Galaxy A70
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core .
- Aina ya Processor (Chipset) – Exynos.
- Uwezo wa GPU – Bado haijajulikana.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine GB 128 huku zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina kuja na RAM ya GB 6 na nyingine GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 32 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2 f/2.2, 12mm (ultrawide) na kamera ya mwisho inakuja na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 4,500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Coral, Black, Blue na White.
- Mengineyo – Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).
Bei ya Samsung Galaxy A70
Kama nilivyo kwambia awali simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi april hivyo bei ya Galaxy A70 pamoja na sifa kamili za simu hii tutazijua siku hiyo. Kuhakikisha haupitwi na habari yoyote kuhusu simu tembelea ukurasa huu pamoja na Tanzania tech kwa ujumla. Pia unaweza kusoma hapa kujua sifa za simu nyingine ya Galaxy A20 iliyo zinduliwa hivi karibuni.