Vodacom Tanzania Kuja na Huduma Mpya ya M-Pesa Fuliza

Huduma hii inatarajiwa kuja Tanzania na nchi nyingine nne
Vodacom Tanzania Kuja na Huduma Mpya ya M-Pesa Fuliza Vodacom Tanzania Kuja na Huduma Mpya ya M-Pesa Fuliza

Hivi karibuni, kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya ilianzisha huduma mpya ya Overdraft iliyopewa jina la Fuliza. Huduma hii inakuwezesha wewe mtumiaji wa M-Pesa kuweza kutumia pesa zaidi ya ulizo nazo kama utakuwa umepungukiwa wakati ukitaka kufanya malipo na M-Pesa.

Yaani kwa mfano, kama ulikuwa unataka kununua muda wa maongezi kupitia M-Pesa na salio lako la M-Pesa halitoshi basi utaweza kuongezewa kiasi kilichopelea na utakuja kulipa endepo tu ukiweka pesa kwenye akaunti yako ya M-Pesa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation, huduma hii inatarajiwa kuja hapa nchini Tanzania siku za karibuni pamoja na nchi nyingine nne ambazo ni Lesotho, Ghana, Congo (DRC) na Mozambique. Huduma hii ya Fuliza ilianzishwa January 5 na kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya kwa ushirikiano na benki za Commercial Bank of Africa (CBA) na KCB Group.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti ya Safaricom, watumiaji wa huduma hiyo wa nchini Kenya wanaruhusiwa kupata mkopo wa hadi KSh 70,000 ambayo hii ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,632,000, huduma hiyo ya Fuliza ni tofauti na mkopo ya kawaida kwani pamoja na vigezo vingine mtumiaji atalipa pesa hizo pale tu anapoweka pesa kwenye akaunti yake.

Kwa sasa bado hakuna ripoti kamili ya lini huduma hii itaanza hapa nchini Tanzania au kama huduma hiyo itautwa Fuliza kama ilivyo kwa upande wa Kenya, Kwa habari zaidi za huduma hiyo na jinsi itakavyo kuwa inafanyakazi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use