Huu Hapa Muonekano wa Giza Kwenye Programu ya WhatsApp

Hivi ndivyo muonekano wa giza kwenye WhatsApp utakavyokuwa
Huu Hapa Muonekano wa Giza Kwenye Programu ya WhatsApp Huu Hapa Muonekano wa Giza Kwenye Programu ya WhatsApp

Kama wewe ni mfuatiliaji wa habari mbalimbali hapa Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua habari kuhusu WhatsApp kuja na sehemu mpya ya Dark Mode au muonekano wa giza kwaajili ya kulinda macho yako wakati wa usiku.

Sehemu hii ni kama ile inayopatikana kwenye tovuti hii na app yetu ya Tanzania Tech, sehemu hii itakusaidia kubadilisha muonekano wa tovuti nzima na kuwa na muonekano mweusi ambao huu ni mzuri zaidi kwaajili ya kulinda macho yako hasa wakati wa usiku. Sasa sehemu kama hii inakuja kwenye programu ya WhatsApp ambayo nayo pia itakupa nafasi ya kuweza kuwasha muonekano huo wa giza ili kuweza kulinda macho yako hasa unapokuwa unachati wakati wa usiku.

Advertisement

Kwa kuwa bado sehemu hii iko kwenye hatua ya majaribio, kupitia tovuti ya WAbetainfo tumefanikiwa kupata picha ambazo zina onyesha muonekano wa programu ya WhatsApp ikiwa sehemu hiyo ya Dark Mode au muonekano wa giza ukiwa umewashwa.

Kwa sasa kama unavyoweza kuna kwenye picha hapo juu, hivyo ndivyo progrmu hiyo ya WhatsApp itakavyokuwa pale sehemu ya Dark Mode itakapo kuwa imewashwa. Mpaka sasa bado hakuna taarifa zaidi za lini sehemu hii itakuja kwenye programu ya WhatsApp ya kawaida, hivyo ili kupata taarifa pale sehemu hii itakapo kuja rasmi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku na tuna ahidi tutakupa taarifa zaidi juu ya sehemu hii.

Kwa sasa, kama unataka kujua zaidi jinsi ya kulinda macho yako yasiharibiwe na mwanga wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta, soma hapa kuhusu sheria ya 20 20 20 ambayo itasaidia kulinda macho yako hasa kama unatumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use