Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix Zero 6 na Zero 6 Pro

Hizi hapa ndio sifa na bei ya Infinix Zero 6 Pro
Sifa na Bei ya Infinix-Zero-6- Pro Sifa na Bei ya Infinix-Zero-6- Pro

Kama tetesi zilivyosema, kampuni ya Infinix siku kadhaa zilizopita imezindua simu mpya ya Infinix Zero 6. Kwa hapa Afrika Infinix Zero 6 Pro imezinduliwa huko nchini Kenya, na ni moja kati ya simu nzuri sana kutoka kampuni ya Infinix.

zero 6 pro

Simu zote mbili zinakuja na sifa zinazo karibiana lakini Infinix Zero 6 Pro inakuja na mambo kadhaa ya zaidi kama vile ukubwa wa ndani pamoja na RAM. Tukiangalia moja kwa moja sifa za Infinix Zero 6 Pro, simu hii inakuja na kioo cha Inch 6.18 chenye resolution ya 2160×1080 Pixels pamoja na teknolojia ya IPS LCD na FHD+.

Advertisement

Kioo hicho kwa juu kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama Top Notch, ukingo ambao una hifadhi sensor mbalimbali pamoja na kamera ya Selfie ya Megapixel 20, Hata hivyo kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 24, na nyingine ikiwa na Megapixel 12. Kamera hizi zote zinakuja na mfumo wa AI ambao unaweza kufanya kamera hizi kujua vitu mbalimbali pale unapo piga picha kama vile chakula, wanyama na vitu vingine kama hivyo.

Zero 6 Kamera

Infinix Zero 6 Pro inaendeshwa na processor ya Snapdragon 636 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 256. Sifa nyingine za Infinix Zero 6 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Zero 6 Pro

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 2160×1080 Pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm Snapdragon 636 (SDM636).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 MP, Low-light Sensor na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye 2PD. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Quad LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3650 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Milan Black na Sapphire Cyan.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Zero 6 Kamera 22

Bei ya Infinix Zero 6 Pro

Kwa sasa simu hii tayari imeingia nchini Kenya na inaweza kupatikana kwa oda kwa Shilingi za Kenya Ksh 32,000 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 750,000. Bei inaweza kuongezeka kwa Tanzania.

4 comments
  1. Nani anaweza nsaidia kupata phone nzuri yenye quality ya infinix ila ya uwezo mzuri kwa laki 2.5Tz money

  2. Kama mim ni mtumiaji mzuri wa Infinix. Kwasasa natumia infinix zero 6 pro , swalilangu nikwamba Je, nikitaka kubadilisha kwenda toleo lambele nikienda kwa mawakala naruhusiwa?? Au ni mpaka ninunue nyingine??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use