Kampuni ya Huawei hivi karibuni imeonekana kuendelea kuzindua simu nyingi kwa mfululizo kwaajili ya kuendelea kushikilia rekodi ya kufanya mauzo kwa wingi iliyowekwa na kampuni hiyo mwaka jana 2018. Sasa katika kuendeleza kasi hiyo hivi karibuni Huawei imezindua simu mpya ya Huawei Y6 Pro (2019).
Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Simu hii mpya ya Huawei inakuja na sifa nzuri pamoja na muonekano mzuri huku ikiwa na kioo cha inch 6.1 chenye teknolojia ya IPS LCD pamoja na HD+. Mbali na kioo simu hii inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm) yenye speed ya Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53. Processor hii inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ROM ya GB 32 ambayo inaweza kuongezwa kwa kutumia memory card ya hadi GB 512.
Kwenye upande wa kamera Huawei Y6 Pro (2019) inakuja na kamera ya moja ya Megapixel 13 ambayo inasaidiwa na Flash ya LED Flash. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 8 ambayo nayo pia hii inasaidiwa na Flash ya LED Flash. Sifa nyingine za Huawei Y6 Pro (2019) ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Huawei Y6 Pro (2019)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.09 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa EMUI 9
- Uwezo wa Processor – Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm).
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – RAM GB 3.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye LED Flash na uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF. Huku ikisaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3020 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, microUSB 2.0.
- Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Midnight Black, Sapphire Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Accelerometer, proximity.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Haina Fingerprint.
Bei ya Huawei Y6 Pro (2019)
Kwa upande wa bei ya Huawei Y6 Pro (2019), simu hii inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $135 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania 314,000 bila kodi. Simu hii kwa sasa inapatikana kwa nchini Philippines huku, bado kukiwa hakuna taarifa za ujio wa simu hii hapa Afrika. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa taarifa pindi simu hii itakapofika hapa Tanzania.
Nauliza je bado huawei Y6 pro 2019 haijafika hapa kwetu Tanzania?