Wakati mkutano wa MWC 2019 ukielekea ukingoni kampuni ya Huawei imezidi kuwa kinara kwa kuonyesha teknolojia bora ya simu kwenye simu yake inayojikunja ya Huawei Mate X.
Kama ulikuwa hujui, kupitia mkutano wa MWC 2019 kampuni ya Huawei ilitangaza ujio wa simu yake ya kwanza inayojikunja ya Huawei Mate X, Simu hii inakuja na teknolojia ambayo inaendana kidogo na ile ya Galaxy Fold ambapo simu hiyo inauwezo wa kuwa table na pia unauwezo wa kuwa simu ya kawaida.
Kwa upande wa sifa Huawei Mate X inakuja na kioo cha inch 8.0 ikiwa imefunguliwa kama tablet, na inch 6.38 ikiwa imekunjwa kama simu ya kawaida. Kioo cha Mate X kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED ambayo inafanya simu hii kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya Milioni 16. Kwa upande wa resolution, Huawei Mate X ikiwa kama tablet inakuja na resolution ya 2480 x 2200 pixels, na ikiwa kama simu ya kawaida inakuwa na resolution ya 2480 x 892 pixel.
Mate X inaendeshwa na processor ya Huawei ya Kirin 980 yenye kusaidiwa na Ram ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 512. Ukubwa huu unaweza kuongezewa na NM card ya hadi GB 256. Kama unajiuliza NM Card sio memory card ile ya kawaida bali hii ni aina mpya ya memory ambayo inatumiwa na Huawei.
Kwa upandw wa kamera Huawei Mate X inakuja na kamera tatu, kamera moja inakuja na Megapixel 40 ambayo ni (Wide Angle Lens), nyingine ina Megapixel 16 ambayo hii ni (Ultra Wide Angle Lens) na kamera ya mwisho ina Megapixel 8 ambayo hii ni (Telephoto). Sifa nyingine za Huawei Mate X ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Huawei Mate X
- Ukubwa wa Kioo – Inch 8 ikiwa Tablet na Inch 6.6 ikiwa kama simu ya kawaida, kioo cha simu hii kina teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 2480 x 2200 pixels ikiwa tablet na 2480 x 892 ikiwa simu ya kawaida.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa EMUI 9.1.1
- Uwezo wa Processor – 2 x Cortex-A76 Based 2.6 GHz + 2 x Cortex-A76 Based 1.92 GHz + 4 x Cortex-A55 1.8 GHz.
- Aina ya Processor (Chipset) – HUAWEI Kirin 980.
- Uwezo wa GPU – Mali-G76.
- Ukubwa wa Ndani – GB 512 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na NM card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele –
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 40 (Wide Angle Lens), nyingine ina Megapixel 16 (Ultra Wide Angle Lens) na ya mwisho ina Megapixel 8 (Telephoto). Kamera zote ni kamera za Leica.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host.
- Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Interstellar Blue.
- Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini moja, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Gravity Sensor, Ambient Light Sensor, Proximity Sensor, Gyroscope, Compass, Fingerprint Sensor, Hall sensor, Barometer, Infrared sensor, colour temperature sensor.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwenye Kioo).
Bei ya Huawei Mate X
Kwa sasa Huawei Mate X bado haijakamilika kwa asilimia 100, hivyo bei yake bado haijajulikana ila kwa mujibu wa Huawei simu hii inatarajiwa kutoka rasmi na kuingia sokoni kwenye nusu ya pili ya mwaka huu 2019. Kujua zaidi pale simu hii itakapo kamilika endelea kutembelea ukuras huu tutakupa habari pindi bei ya simu hii itakapo tangazwa.