Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A50 na Galaxy A30

Hizi hapa ndio Simu mpya za Samsung za daraja la kati
Sifa na bei ya Galaxy A30 na Galaxy A50 Sifa na bei ya Galaxy A30 na Galaxy A50

Wakati macho yote yakiwa kwenye mkutano wa MWC 2019, Huku duniani kampuni ya Samsung inaendelea na harakati zake kama kawaida. Hivi karibuni kampuni hiyo imetambulisha simu zake mpya za daraja la kati kama ilivyo semekana kwenye tetesi wiki iliyopita, Galaxy A50 na Galaxy A30 ndio majina ya simu hizo mpya ambazo zinasemekana eti!! kuwa za bei nafuu kutoka Samsung.

Galaxy A30 ndio toleo la bei rahisi zaidi..!!.. kwani simu hii inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels pamoja na teknolojia ya Super AMOLED. Kioo hicho kwa juu kinakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 16.

Advertisement

Tukiwa bado tupo kwenye kamera, Galaxy A30 inakuja na kamera mbili kwa nyuma kamera ambazo maja wapo ina uwezo wa Megapixel 16 na nyingine ina uwezo wa Megapixel 5. Kamera zote zina uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps. Mbali na yote hayo, Galaxy A30 inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi hivyo imepewa alama ya IP68 hii ikiwa na maana simu hii inaweza kukaa kwenye maji ya Mita 1.5 kwa muda wa dakika 30.

Kwenye upande wa processor Galaxy A30 inakuja na processor ya Exynos 7885 Octa (14 nm) yenye kusaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 3, pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 64 au GB 32. Vilevile ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa memory card hadi ya GB 512. Sifa nyingine za Galaxy A30 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A30

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7885 Octa (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G71.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A30

Kwa upande wa bei ya Galaxy A30 bado bei yake haijajulikana rasmi lakini nikwambie tu simu hii haitakuwa ya bei rahisi kiasi hicho. Kwa makadirio simu hii inaweza kuuzwa kuanzia dollar za marekani $400 sawa na Tsh 938,000 bila kodi. Kumbuka bei hii ni ya kukadiria hivyo bei inaweza kubadilika pale bei halisi itakapo tangazwa.

Kwa upande wa Galaxy A50, simu hii pia inakuja na kioo sawa na Galaxy A30 lakini simu tofauti yake iko kwenye processor. Galaxy A50 inakuja na processor ya Exynos 9610 Octa inayosaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128 au GB 64. Ukubwa wa simu hii unaweza kuongezwa na Memory card hadi ya GB 512.

Mbali na hayo Galaxy A50 inakuja na kamera tatu kwa nyuma, moja ikiwa na Megapixel 25 nyingine ina Megapixel 8 na nyingine ina Megapixel 5. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 25 yenye teknolojia ya HDR pamoja na uwezo kurekodi video za 1080p@30. Sifa nyingine za Galaxy A50 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy A50

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, pamoja na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Cortex-A73 & 6×1.6 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9610 Octa.
  • Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 128 na nyingine inayo GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 25 yenye f/1.7, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, (ultrawide), na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy A50

Kwa sasa bei ya Galaxy A50 bado haijajulikana, ila unaweza kuipata simu hii kwa bei ya makadirio kuanzia dollar za marekani $500 sawa na Tsh 1,173,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka au kupungua pale bei rasmi itakapo tangazwa.

Hizo ndio sifa pamoja na bei ya makadirio ya simu hizi mpya za Galaxy A30 na Galaxy A50. Kujua zaidi kuhusu simu hizi unaweza kusoma zaidi hapa.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use