Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Picha ya Simu Mpya ya Nokia 9 PureView Yenye Kamera Tano

Huu ndio muonekano halisi wa simu mpya ya Nokia 9
Picha ya Simu Mpya ya Nokia 9 PureView Yenye Kamera Tano Picha ya Simu Mpya ya Nokia 9 PureView Yenye Kamera Tano

Kampuni ya Nokia inatarajia kuzindua simu yake mpya ya Nokia 9 Pureview, Simu hii inatarajia kuwa moja kati ya simu bora ya Nokia kwa mwaka huu 2019. Hata hivyo ubora wa simu hii haupo kwenye muonekano wake bali upo kwenye aina yake ya kamera hasa za nyuma kwani simu hii inakuja na kamera tano za nyuma.

Kwa sasa bado hakuna anayejua kuhusu kamera hizo zinavyofanya kazi ila inasemekana kamera hizo zitakuwa na uwezo mkubwa kuliko simu nyingine za Nokia ambazo zimewahi kutoka hadi sasa. Mbali na hayo simu hii ndio inatarajiwa kuwa simu ya kwanza yenye idadi kubwa ya kamera kwa nyuma.

Advertisement

nokia 9 pureview

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hiyo hapo juu, idadi ya kamera kwa nyuma ni kamera tano huku kukiwa na flash iliyoko upande wa kushoto juu, pamoja na sensor maalum ambayo iko juu upande wa kulia. Kwa mujibu wa mtandao wa 91mobile hii picha yenye muonekano halisi wa simu hiyo ya Nokia 9 Pureview.

Mbali na kamera simu hii inatarajiwa kuja na muundo wa kawaida huku ikiwa na ukingo wa juu na chini, pamoja na sehemu ya fingerprint juu ya kioo kama inavyo onekana kwenye picha nyingine hapo chini.

Picha Nokia 9 Pureview

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, Nokia 9 Pureview inatarajiwa kuja na kioo cha inch 5.99 ambacho kitakuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, huku kikiwa na resolution ya 1440 x 2960 pixels. Mbali na yote Nokia 9 inasemekana kuja na teknolojia za kuzuia maji na vumbi au (IP68 dust/water proof) yenye uwezo wa kufanya simu hiyo kukaa kwenye maji yenye urefu wa mita 1.5 kwa dakika 30.

Sifa nyingine zinazotarajiwa kwenye Nokia 9 Pureview ni pamoja na processor ya Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm), yenye speed ya Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver), pamoja na ukubwa wa ROM au ukubwa wa ndani wa GB 128 vyote vikiwa vinasidiwa na RAM ya GB 6.

Simu hii inatarajiwa kuja na battery kubwa ya Li-Po 4150 mAh yenye uwezo wa kukaa na chaji kuanzia siku mbili au tatu kulingana na matumizi yako. Pia Nokia 9 Pureview inasemekana kuja na teknolojia ya Fast charge hivyo utaweza kuchaji battery ya simu hii kwa asilimia 50 kwa muda wa dakika 15.

Kwa sasa hayo ndio machache kuhusu simu hii mpya ya Nokia, kujua zaidi kuhusu simu hii mpya ya Nokia hakikisha unaungana nasi kwenye mkutano wa MWC 2019 ambao unatarajia kuanza rasmi tarehe 25 mwezi huu, ambapo kampuni ya Nokia na kampuni nyingine nyingi zitakuwa zikionyesha bidhaa zake mpya kabisa kwa mwaka 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use