Mitandao Kama YouTube ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Mitandao hii itakusaidia kupata pesa mtandaoni bila masharti magumu
pesa mtandao kwa mitandao kama youtube pesa mtandao kwa mitandao kama youtube

YouTube ni moja kati ya mitandao mikubwa ambayo imekwepo kwa muda mrefu sasa, mtandao huu umekuwa msaada kwa watu wengi pamoja na biashara mbalimbali kote duniani kutokana na mfumo wake wa kulipa watumiaji wa mtandao huo kutokana na matangazo mbalimbali ya biashara yanayo onekana kwenye video hizo.

Siku za karibuni YouTube imeongeza vigezo na masharti juu ya jinsi unavyoweza kupata pesa kupitia mtandao huo, masharti hayo kwa wengine yamekuwa ni magumu hasa pale mtu anapokuwa anataka kuanza kutumia mtandao huo kwa ajili ya kutafuta kipato. Kutokana na ugumu huo pamoja na vikwanzo hivyo wengi wamekuwa wakikata tamaa na kujikuta wakishndwa kabisa kuanza kupata pesa mtandaoni kupitia YouTube.

Kutokana na hilo, leo hapa Tanzania Tech tunakuletea aina za tovuti ambazo zinafanana kabisa na YouTube ambazo unaweza kutumia kupata pesa mtandaoni kama ilivyo mtandao wa YouTube. Kumbuka unachotakiwa kifanya ni kuweka video ambazo ndizo ndio zitakusaidia kupata pesa mtandaoni kwa urahisi. Haijalishi kama wewe ni mpenzi wa game, filamu, muziki au vichekesho mitandao hii itakusaidia sana kutengeneza pesa mtandaoni.

Advertisement

DTube

Mitandao Kama YouTube ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni

Dtube ni mtandao kama youtube ambao unakulipa pesa kutoka na watumiaji wa mtandao huo kuangalia sana video yako pamoja nakupenda zaidi video yako. Mtandao huu unakulipa kwa pesa taslim kupitia bank au kwa pesa za kidigital Cryptocurrency. Kujiunga na mtandao wa DTube ni rahisi sana unacho takiwa ni kutengeneza akaunti na kuanza kuweka video zako mara moja.

JIUNGE HAPA

BridTV

BridTV-696x327

BridTV ni mtandao mwingine ambao unaweza kusaidia kupata pesa mtandaoni kwa kuweka video zako kwenye mtandao huo, Mtandao huo una kusaidia kupata zaidi ya asilimia 50 ya mapato unayo tengeneza kutokana na matangazo yanayo onekana kwenye video zako. Mtandao huu nao pia ni rahisi kujiunga na unaweza kujiunga kwa kutengeneza akaunti yako kupitia link hapo chini.

JIUNGE HAPA

DailyMotion

DailyMotion-696x295

Dailymotion ni moja kati ya mtandao ambao upo kwa muda mrefu sana, mtandao huu ni moja ya kati ya mitandao ambayo ni washindani wa mtandao wa YouTube. Mtandao huu unaweza kusaidia wewe kupata pesa mtandaoni kwa kuweka video zako kwenye mtandao huo, unaweza kulipwa kutokana na watu wengi kutazama video yako zaidi na kubofya matangazo yanayopita pembeni au baada au katikati ya video. Unaweza kujiunga na Dailymotion kwa kubofya hapo chini.

JIUNGE HAPA

Twitch

Twitch-696x317

Twitch ni moja kati ya mitandao ya siku nyingi na pia huu ni moja kati ya mitandao ambayo iko kwenye list ya mitandao inayo shindana na mtandao wa YouTube. Mtandao huu ni kama YouTube lakini Twitch inapendwa zaidi na wachezaji wa game, ili kupata pesa nyingi kupitia mtandao huu ni vizuri kuweka video ambazo zinaonyesha jinsi unavyocheza game na inatakiwa uwe na uwezo wa kucheza game hizo. Pia unaweza kuonyesha video live ukiwa unacheza game hiyo na utaweza kulipa moja kwa moja na watazamaji, kama wewe ni mpenzi wa game na ungependa kutengeneza pesa mtandaoni basi Twitch ni moja ya mtandao wa muhimu kwako.

JIUNGE HAPA

Facebook for creators

Facebook-for-creators-696x311

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook basi ni lazima utakuwa unajua kuhusu hii, kama hujui basi ngoja nikufahamishe hapa. Facebook wanakupa uwezo wa kutengeneza pesa kupitia akaunti yako ya Facebook kwa kuweka video mbalimbali. Video hizo zinatakiwa kuwa zako kwa asilimia 100 pamoja na nyimbo zilizopo ndani ya video hizo, kujiunga na mtandao huo ni rahisi sana kama tayari unayo akaunti ya Facebook kupitia kompyuta yako bofya link hapo chini.

JIUNGE HAPA

Viddler

Viddler-696x348

Viddler ni mtandao mwingine ambao utakusaidia kutengeneza pesa mtandao kwa kutumia video, kwa kutumia mtandao huu unaweza kutengeneza pesa mtandaoni kwa kuweka video zako kwenye mtandao huu na kuweza kupata pesa kutokana na matangazo mbalimbali kwenye video zako. Kujiunga na mtandao huu ni rahisi sana na unatakiwa kutengeneza akaunti kwa kutumia link hapo chini.

JIUNGE HAPA

Na hizo ndio baadhi ya tovuti ambazo zinafanana na YouTube ambazo unaweza kuzitumia kupata pesa mtandaoni, kama unataka kujifunza zaidi kuhusu kupata pesa mtandaoni hakikisha upitwi na makala kama hizi hapa Tanzania Tech, kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Pia kama umekwama sehemu yoyote unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

8 comments
  1. Habari ndugu zangu, najaribu kujiunga, ninatumia njia takribani zote lakini bado kuna ugumu nauona kwenye ku-upload Video nashiundwa maana kuna option za FREE, BASIC na CUSTOM, na hapo ndipo ninapoanza kuona ugumu wa kutokuelewa wapi napaswa kuanzia.
    Naitaji msaada wa maelezo zaidi juu ya hilo.

  2. Habari naitwa hamenya
    Naomba kufahamu kuhusu app ya twitch ambayo unaweza kulipwa kwa kucheza game
    Je inafanya kazi ata kwa simu za android, napata pesa kwa njia ipii

  3. Maoni*haya maelekezo ni machache sana ni vigumu mtu kuelewa kwa ufasaha koz shida inakuja kwenye kutengeneza pesa ,, unajisajili vp ! yani uko kwa makampuni yanayodili na mchakato wa pesa ! kulipa

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use