Baada ya kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya za Galaxy M10 na Galaxy M20, hivi karibuni kampuni hiyo inatarajiwa kuzindua simu mpya za Galaxy A50, Galaxy A30 na Galaxy A10 zote zikiwa kama simu za daraja la kati (mid-range lineup) kutoka Samsung.
TABLE OF CONTENTS
Samsung Galaxy A10
Kwa mujibu wa tetesi zilizotolewa hivi karibuni na tovuti ya GSM Arena, kati ya simu zote hizi simu itakayokuwa ya bei nafuu zaidi kuliko zote ni Galaxy A10. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Simu hiyo inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye teknolojia ya HD+, vilevile Galaxy A10 inakuja na kamera moja kwa nyuma yenye Megapixel 13 na kamera moja ya Selfie yenye Megapixel 5.
Galaxy A10, itakuwa inaendeshwa na processor ya Exynos 7884B Octa core 1.6GHz, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ROM ya GB 32. Simu hii inatajwa kuwa na battery kubwa ya 4000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku mbili kulingana na matumizi yako.
Samsung Galaxy A30
Kwa upande wa Galaxy A30, Simu hii inasemekana kuja na kioo cha inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED pamoja na resolution ya 1080 x 2340 Pixel. Galaxy A30 inatarajiwa kuja na kamera mbili kwa nyuma, huku moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 16.
Mbali na hayo simu hii inasemekana kuendeshwa na processor ya Exynos 7904 Octa core 1.8GHz, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 au GB 4 pamoja na ROM ya GB 32 au GB 64, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card ya hadi GB 512.
Kwa upande wa Battery Galaxy A30 inatarajiwa kuja ikiwa na Battery yenye ukubwa wa 4000 mAH yenye teknolojia ya Fast Charging ambayo inaweza kuchaji simu hii hadi asilimia 50 ndani ya dakika 15.
Samsung Galaxy A50
Galaxy A50 yenyewe ndio inasemekana kuwa simu ya bei ghali kidogo kwenye simu hizi, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye teknolojia ya Super AMOLED pamoja na resolution ya 1080 x 2340 Pixel. Simu hii inakuja na kamera tatu kwa nyuma, moja ikiwa na Megapixel 25 nyingine ikiwa na Megapixel 5 na nyingine ikiwa na Megapixel 8, kwa mbele Galaxy A50 inakuja na kamera moja ya Selfie yenye Megapixel 25.
Mbali na yote hayo Galaxy A50 inasemekana kuja na processor ya Exynos 9610 Octa core 2.3GHz ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 au GB 6 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 32 au GB 64 au GB 128, simu zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa kiasi cha ROM na Memory card hadi ya GB 512.
Kama ilivyo Galaxy A30, Galaxy A50 nayo inakuja na battery yenye uwezo wa 4000 mAH yenye teknolojia ya Fast Charging ambayo inaweza kuchaji simu hii hadi asilimia 50 ndani ya dakika 15.
Kwa sasa simu hizi bado hazijatangazwa zitatoka lini ila kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, simu hizi zinatarajiwa kutoka kuanzia mwezi ujao. Kwa habari zaidi za simu hizi pamoja na kujua zaidi sifa za simu hizi, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.