Watumiaji wa Android Kutumia Alama za Vidole Kufungua Akaunti

Sasa ingia kwenye akaunti zako mtandaoni kwa kutumia alama za vidole
Watumiaji wa Android Kutumia Alama za Vidole Kufungua Akaunti Watumiaji wa Android Kutumia Alama za Vidole Kufungua Akaunti

Kama inavyojulikana ni watu wengi sana duniani na hasa hapa kwetu Tanzania hawapendi kufungua akaunti mtandaoni ili kupata huduma fulani, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda usalama wa mtandao umekuwa ni mdogo sana kiasi kwamba imekuwa ni lazima kufungua akaunti ili kuweza kupata huduma mtandaoni.

Lakini katika kurahisisha mambo hivi karibuni watumiaji wa simu za Android wataweza kutengeneza akaunti au kuingia kwenye akaunti zao za mitandao mbalimbali kwa kutumia alama za vidole a.k.a Fingerprint. Hayo yamebainika baada ya ripoti mpya kutoka FIDO Alliance, iliyokuwa ikisema kuwa mfumo wa Android sasa umepewa uthibitisho wa kutumia mfumo wa FIDO2 (FIDO2 Certified), uthibitisho ambao una tambua na kuruhusu mfumo wa Android kuweza kutumia ulinzi wa alama za vidole ndani ya app pamoja na tovuti mbalimbali.

Watumiaji wa Android Kutumia Alama za Vidole Kufungua Akaunti

Advertisement

Mfumo wa ulinzi wa FIDO2 unasaidia watumiaji wa vifaa mbalimbali kutumia ulinzi uliopo ndani ya vifaa husika (Fingerprint, Face ID, Bluetooth, Wifi, USB) kuweza kufungua akaunti kupitia tovuti au apps ambazo zimewezeshwa na ulinzi huo bila kutumia mfumo ule wa kuandika username pamoja na password.

Kifupi ni kuwa, kama unataka kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook, unachotakiwa kufanya ni kuweka alama yako ya kidole (Fingerprint) kwenye simu yako pale unapofika kwenye ukurasa wa kuingia (Login) na moja kwa moja utaingia kwenye akaunti yako bila kujaza password wala username kwenye fomu maalum ya mtandao husika.

Mfumo huu wa FIDO2 unatumia mifumo mipya ya ulinzi ya W3C’s Web Authentication specification pamoja na Client to Authenticator Protocol (CTAP), ambayo yote ni mifumo ya ulinzi kutoka FIDO Alliance. Kwa sasa mifumo yote hii inaweza kufanya kazi kwenye kivinjari cha Firefox, Chrome,  Microsoft Edge huku ikifanyiwa majaribio kwenye kivinjari cha Safari.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa mfumo umesha kamilika kilichobaki ni wabunifu wa programu kuweka mfumo huo kwenye apps zao pamoja na tovuti zao na moja kwa moja watumiaji wa Android na vifaa vingine vyenye kusapport vitaweza kufanya kazi. Kwa sasa inasemekana ili kuweza kutumia sehemu hiyo itakapo kujua, simu yako inatakiwa kuwa na mfumo wa Android 7.0 na kuendelea.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use