Samsung Yazindua Space Monitor Kioo Kipya cha Kompyuta

Kioo kipya cha Samsung chenye kuchukua nafasi ndogo ya meza yako
Samsung Yazindua Space Monitor Kioo Kipya cha Kompyuta Samsung Yazindua Space Monitor Kioo Kipya cha Kompyuta

Wakati tukikaribia kwenye mkutano wa CES 2019, Kampuni ya Samsung imeanza mapema kwa kutangaza ujio wa kioo kipya cha kisasa kwaajili ya kompyuta. Kioo hicho kinachoitwa Samsung Space Monitor, kimetengenezwa maalum kwaajili ya kutoshea kwenye meza ndogo au kwa mtu ambaye anapenda kupata nafasi kubwa ya meza pale anapokuwa hatumii kompyuta.

https://youtu.be/MXYEscjS1a8

Samsung Space Monitor imetengenezwa na mkono maalum ambao huu ufungwa kwenye meza na pale unapotaka kutumia kioo hicho unaweza kuvuta kioo hicho kwa mbele na mkono huo hujikunja ili kioo hicho kiweze ku-kufikia. Vilevile mkono huo ambao pia huficha nyaya ambazo mara nyingi uchukua nafasi kubwa pale mtu anapokuwa anatumia kioo cha kompyuta.

Advertisement

Samsung-2019-Monitors_main_1-min

Samsung Space Monitor inakuja kwa size mbili tofauti, kioo cha inch 27 chenye QHD resolution na kioo cha inch 34 chenye teknolojia ya 4K UHD. Kioo hicho pia kinakuja na sehemu ya HDMI pamoja na viunganishi vya USB pamoja na power cable.

Samsung Yazindua Space Monitor Kioo Kipya cha Kompyuta

Kwa sasa bado Samsung haijatangaza bei ya kioo hicho, kujua zaidi kuhusu kioo hichi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuwa mubashara kwenye mkutano wa CES 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use