in

Kujua Muda Gani wa Kupost Kwenye Akaunti Yako Instagram

Jifunze hapa hatua kwa hatua jinsi ya kujua muda halisi wa kupost Instagram

Kujua Muda Gani wa Kupost Kwenye Akaunti Yako Instagram

Siku hizi mtandao wa Instagram umekuwa ndio mtandao muhimu kwa ajili ya kutafuta masoko mbalimbali hasa kwa wafanya biashara wakubwa na hata wale wadogo. Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa mtandaoni na unayo akaunti ya instagram ya kibiashara basi makala hii ni kwa ajili yako.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia ambayo unaweza kuitumia ili kuweza kujua muda gani ambao unaweza kupost kwenye akaunti yako ya mtandao wa Instagram, kumbuka kila akaunti inakuwa na muda wake maalum hivyo ni vyema kufuata hatua hizi kwenye akaunti yako ili kuweza kujua muda ambao watu wengi zaidi wanaweza kuona post yako.

Mbali na hayo kupitia makala hii utaweza kujifunza ni siku gani katika wiki ambayo watu wengi zaidi wana uwezekano wa kuona post zako kwenye akaunti yako, hii itakusaidia kuweza kupanga post za kupost siku hiyo na kuweza kuwafikia wateja wako wengi zaidi, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hii rahisi.

Mahitaji

Kwanza kitu cha muhimu unachohitaji ni akaunti ya Instagram ambayo inatumika au ilikuwa inatumika kwa muda mrefu kidogo, kitu kingine unatakiwa kuhakikisha akaunti yako ni ya kibiashara yaani (Business Account), kama akaunti yako bado ni personal account unaweza kubadilisha na kuwa akaunti ya kibiashara kwa kufuata maelezo kwenye ukurasa huu hapa.

kubadilisha akaunti ya Instagram

Jinsi ya Kupata Data za Akaunti Yako

Baada ya kubadilisha akaunti yako ya kawaida kuwa ya kibiashara sasa endelea kwa kufungua akaunti yako ya Instagram kisha bofya mishale mitatu iliyopo juu upande wa kulia, baada ya hapo chagua sehemu iliyo andikwa Insights.

sehemu ya insights instagram

Baada ya kufungua sehemu hiyo sasa utapelekwa kwenye ukurasa wenye data za muhimu ambazo zitaenda kusaidia wewe kujua ni muda gani wa kupost kwenye akaunti yako ya Instagram, pia data hizi zitakusaidia kujua siku nzuri za kupost kwenye akaunti yako pamoja na mambo mengine mbalimbali.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Microphone

Kujua Watu Wanaotembelea Akaunti Yako

Kwanza tuangalie jinsi ya kujua watu wanao tembelea akaunti yako ya Instagram, hapa unaweza kuangalia kati ya wanaume au wanawake, pia unaweza kuangalia ni mkoa gani ambao watu wana angalia akaunti yako zaidi.

Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye ukurasa wa insight kama nilivyo kuonyesha hapo juu, kisha chagua sehemu ya Audience ambayo iko juu upande wa kulia ndani ya ukurasa wa insights.

sehemu ya audience instagram

Baada ya kubofya hapo sasa uko kwenye ukurasa ambao tutakuwa tunazungumzia kwa siku ya leo hivyo kila kitu ambacho tunahitaji kitakuwa kwenye ukurasa huu, basi baada ya hapo sasa ni wakati wa kuangalia ni mkoa gani watu wanao tembelea zaidi akaunti yako ya Instagram.

Kwa kushuka chini kidogo sehemu ya Top locations utaona data zinazo kuonyesha ni mkoa gani ambao watu wengi zaidi huangalia au kutembelea ukurasa wako wa Instagram, kwa kubofya sehemu ya Countries utaweza kuona nchi ambazo watu wengi zaidi hutembelea ukurasa wako. Kumbuka, mkoa au nchi illiyotangulia juu na yenye mstari wa blue mrefu zaidi ndio mkoa au nchi inayoongoza kwa watu kutembelea akaunti yako ya Instagram.

sehemu ya location instagram

Kwenye umri au Age Range pia ni hivyo hivyo unaweza kuona umri wa watu wanaotembelea zaidi akaunti yako ya Instagram, hii itakusaidia zaidi kujua ni kitu gani cha kupost kwa ajili ya watu hao. Pia unaweza kuangalia idadi hiyo kwa jinsi kwa kuchagua sehemu ya Men au Women iliyoko pembeni ya sehemu ya Age Range kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.

Jinsi ya Kujua Muda Gani wa Kupost

Sasa kama unataka kujua ni muda gani wa kupost au kama unataka kujua siku gani ni nzuri kwa kupost basi hii ni hatua muhimu kwako. Unacho takiwa kufanya ni kushuka chini kabisa ya ukurasa wa Insight, hapo utaona sehemu iliyo andikwa Followers, sehemu hii itakupa data za muhimu za kuweza kujua muda gani au siku gani nzuri ya kupost zaidi kwenye akaunti yako.

Jinsi ya Kujiweka kwenye Google Search Kama Mtu Maarufu

Kwa kubofya sehemu ya Hours utaweza kuona msaa ambayo ni mazuri zaidi kwa wewe kupost, hii ni muhimu kwani itakuwa inaonyesha data ambazo zinaonyesha muda ambao watu wengi zaidi wanao kufuata wanakuwa online. Kama ilivyo kwenye hatua ambazo zimemita kwa kuangalia mstari wa blue uliozidi nio masaa mazuri ya kupost na ndipo muda ambao follower wako wengi zaidi huwa online.

sehemu ya Followers Instagram

Kama unavyoweza kuona muda ambao watu followers wengi wa tanzania tech huwa hewani ni kati ya saa kumi na mbili ya jioni hadi saa tatu ya usiku ambapo watu wengi ndio huwa hewani zaidi.

Hivyo basi kama unavyoweza kuona hii itakusaidia kuweza kupost muda ambao watu wengi zaidi huwa hewani, unaweza kuangalia data hizi kila mwezi ili kuweza kujua mabadiliko ya tabia za watu walio kufuata kwenye akaunti yako ya Instagram.

Kwa upande wa siku nayo ni hivyo hivyo, unaweza kuona siku ambayo watu wengi zaidi walio kufuata wako hewani kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.

sehemu ya followers instagram

Kama unavyoweza kuona hapo juu, siku ambayo wafuasi wengi wa Tanzania Tech wako hewani ni siku ya jumamosi, unaweza kuona kwa kuangalia mstari wa blue ambao unaonyesha siku kwa chini.

Kwa kutumia njia hizi utaweza kujua ni muda gani wa kupost zaidi kwenye akaunti zako za mtandao wa Instagram, kama nilivyo kwambia awali data hizi ni tofauti kwa kila akaunti hivyo ni vyema kuangalia kwenye akaunti yako kuweza kujua mambo mengi kuhusu akaunti yako. Pia njia hii ni nzuri zaidi kama ukitumia kuongeza nguvu kwenye kupost siku na masaa usika na sio kuacha kupost kabisa kwenye siku ambazo hakuna watu wengi.

Hadi hapo natumaini njia hii itaendelea kusaidia kukuza biashara yako na kufanya upate wateja zaidi kwa kupost kwa muda sahihi pale watu wanapo kuwa online. Kama kuna mahali ujaelewa au kama unayo maswali au maoni unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maoni 1

Toa Maoni Hapa

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.