Kampuni maarufu ya kutengeneza simu ya Xiaomi yenye makao yake makuu huko nchini China, hivi karibuni imeanza kujiandaa kuangalia rasmi soko la simu nchini Afrika. Kwa mujibu wa tovuti ya Tech in Asia, Xiaomi inategemea kufungua idara maalum barani afrika, idara ambayo itakuwa inaongozwa na makamu wa raisi wa sasa wa Xiaomi, Manu Kumar Jain.
Kampuni ya Xiaomi ilianzishwa mwaka 2010 na Lei Jun, Kutokea kipindi hicho hadi sasa kampuni ya Xiaomi imekuwa ni kampuni maarufu kwa kuuza simu za bei nafuu ingawaje siku za karibuni kampuni hiyo imeonekana kujaribu kutengeneza simu za gharama za daraja la kati.
Endapo kampuni ya Xiaomi ikifanikiwa kuja Afrika, itakuwa ni moja kati ya kampuni za China ambazo ziko kwenye list ya kampuni zinazo uza simu za bei nafuu hapa Afrika. Transsion ndio jina la kampuni mama inayo miliki bidhaa za TECNO, Infinix na iTel, kampuni hiyo sasa ndio inayoongoza kwa kuuza simu za bei nafuu barani Afrika huku asilimia 38 ya mauzo yote duniani kutoka kampuni hiyo yakiwa yanatokea Afrika.
Kampuni ya Xiaomi inamiliki bidhaa nyingine kama Redmi, sehemu ya kampuni hiyo inayotengeneza simu za bei nafuu zaidi, pamoja na Xiaomi TV sehemu ya kampuni hiyo ambayo imeanzishwa hivi karibuni ambayo inahusika na utengenezaji wa Smart TV au TV Janja.
Kwa sasa Xiaomi ni moja kati ya kampuni zinazo kuwa kiteknolojia, hivi karibuni mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo alionyesha teknolojia mpya ya Fingerprint ambayo kampuni hiyo inategeneza, pia kampuni hiyo siku kadhaa zilizopita ilionyesha aina mpya ya simu ambayo inayojikunja ambayo pengine inategemewa kuja siku za karibuni.
Kwa sababu ya kukuwa huko kwa teknolojia ya utangenezaji simu kutoka kampuni ya Xiaomi ni wazi kampuni kama TECNO na makampuni mengine ya utengenezaji simu hapa Afrika yatakuwa na wakati mgumu pale kampuni hiyo itakapo kuja hapa Afrika na kufanikiwa kuuza simu za bei nafuu kama ilivyo kampuni ya TECNO na Infinix.
Nini maoni yako kwenye hil..? Je unaonaje kuhusu ujio wa kampuni ya Xiaomi hapa Afrika, je ungependa kumiliki simu za Xiaomi za bei nafuu kuliko simu za Tecno..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.