Mwaka 2019 tayari umesha anza rasmi na kwenye ulimwengu wa teknolojia tunapata nafasi ya kuweza kuanza upya na kuangalia kwa jinsi gani teknolojia imekuwa kwa mwaka 2019. Kama kawaida 2019 utakuwa ni mwaka wa Smartphone kwani kwenye ulimwengu huu ndipo kampuni nyingi zinaonekana kuweka macho zaidi. Kudhitbitisha haya, leo nimekuandalia list ya simu ambazo pengine unaweza kuziona kipindi cha mwanzoni mwa mwaka 2019.
1. Nokia 9 View
Inatarajiwa Mwezi January
Nokia 9 View ni simu mpya kabisa kutoka kampuni ya Nokia, Simu hii inatazamiwa kutoka mwishoni mwa mwezi Januari. Kama unavyoweza kuona moja ya kitu ambacho kinasubiriwa kwa hamu kwenye simu hii ni uwezo wake wa kuwa na kamera 5 kwa nyuma pamoja na sehemu ya fingerprint juu ya kioo.
Simu hii imesha zinduliwa rasmi na unaweza kusoma hapa kujua mengine zaidi kuhusu simu hii ikiwa pamoja na sifa zake – SOMA HAPA.
2. Samsung Galaxy S10
Inatarajiwa Mwezi February
Simu nyingine ambayo inasubiriwa kwa hamu sana na watu wengi ni Samsung Galaxy S10, Simu hii inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi February. Kikubwa kuhusu simu hii mpya ni muundo wake mpya ambao unatarajiwa kuwa wa kisasa kabisa tofauti na simu nyingine za Galaxy S zilizotoka miaka iliyopita. Kingine ni mfumo wa Samsung One UI, mfumo mpya ambao unatarajiwa kuwa wa tofauti kabisa kwenye simu za Samsung.
Simu hii imesha zinduliwa rasmi na unaweza kusoma hapa kujua mengine zaidi kuhusu simu hii ikiwa pamoja na sifa zake – SOMA HAPA.
3. Samsung Inayojikunja
Inatarajiwa Mwezi February
Kampuni ya Samsung inasemekana kuwa ya kwanza mwaka huu kutoa simu yake ya kwanza ambayo inakuja na uwezo wa kuwa simu ya kawaida na kuwa tablet. Simu hii ambayo bado haijajulikana jina lake, inatarajiwa kutoka au kuzinduliwa siku mmoja na simu mpya ya Galaxy S10. Yako mengi ambayo hatuyajui kuhusu simu hii, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.
Simu hii imesha zinduliwa rasmi na unaweza kusoma hapa kujua mengine zaidi kuhusu simu hii ikiwa pamoja na sifa zake – SOMA HAPA.
4. Huawei P30
Inatarajiwa Mwezi March
Huawei imefanikiwa sana mwaka huu kwa kuwa kampuni ya pili kwa mauzo ya simu kwa mwaka 2018. Lakini ni wazi mafanikio haya yametokana na simu mpya ya Huawei P20 na P20 Pro ambazo simu hizi zinasemekana kuwa moja ya simu zenye kamera nzuri kwa mwaka 2018. Kwa upande mwingine Huawei inatarajia kuja na simu yake mpya ya Huawei P30 mwezi wa tatu mwaka huu 2019. Pia inasemekana Huawei inajiandaa kuja na simu yake ambayo nayo inajikunja kama ilivyo ile ya Samsung.
5. Google Pixel 3 Lite
Inatarajiwa Mwezi March
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali, Inasemekana kampuni ya Google inatarajia kuja na toleo la bei rahisi la simu za Google Pixel 3 Lite, toleo ambalo linasemekana kuwa bora zaidi kwenye kamera kwa simu za bei rahisi za mwaka 2019. Simu hii inatarajiwa kutoka katikati ya mwezi wa tatu mwaka huu 2019.
6. Sony Xperia XZ4, Xperia XZ4 Compact, XA3, XA3 Ultra
Inatarajiwa Mwezi March au February
Mwaka 2018 haukua mwaka mzuri sana kwa kampuni ya Sony, Lakini labda mwaka 2019 unatarajiwa kuwa mwaka wa Sony kwani inajiandaa kuja na simu zenye uwezo mkubwa sana wa kamera. Kama ulisha wahi kutumia simu ya Sony basi lazima unakubaliana na mimi kuwa Sony iko vizuri sana hasa kwenye utengenezaji wa kamera nzuri. Kwa sasa bado hakuna tarehe sahihi ya kutoka kwa simu hizi ila inasemekana simu hizi kutoka mwezi February au mwishoni mwa mwezi wa tatu.
Simu hii imesha zinduliwa rasmi na unaweza kusoma hapa kujua mengine zaidi kuhusu simu hii ikiwa pamoja na sifa zake – SOMA HAPA.
7. One Plus 7
Inatarajiwa Mwezi May
Mwaka 2018 ulikuwa ni mwaka mzuri sana kwa kampuni ya One Plus, Kampuni hii ilifanikiwa kushika macho ya watu wengi duniani kwa simu yake ya One Plus 6 kuwa kwenye list ya simu bora zaidi kwa mwaka 2018. Simu hii inatarajiwa kuja mwezi May na kutokana na uwezo wa simu hii ya One Plus 6 ni wazi kuwa One Plus 7 itakuwa simu bora zaidi.
Na hizo ndio simu ambazi zinatarajiwa mwanzoni mwa mwaka huu 2019, Kujua zaidi kuhusu simu hizi hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku. Kwa habari za haraka zaidi za Teknolojia Download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store na App Store.
Naomba bei za simu na Aina za simu kupitia namba yangu ya WhatsApp 0693435138