Kampuni ya Samsung iko mbioni kutoa simu yake mpya ya Samsung Galaxy S10 ambayo itakuwa ni toleo la maboresho la simu ya Samsung Galaxy S9. Japo kuwa Galaxy S10 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwaka 2019 lakini tayari tetesi mbalimbali za simu hii zimeanza kuzuka mtandaoni. Kuyaona hayo leo nimekusanya tetesi zote za muhimu kuhusu simu hii mpya.
Muundo wa Galaxy S10
Kwa upande wa muundo Galaxy S10 inatarajiwa kuwa simu ya tofauti kabisa na Galaxy S9. Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali Galaxy S10 inatarajiwa kuja na kioo kikubwa zaidi ambacho ni Full Display, japo kuwa simu nyingi mwaka 2018 zime kuwa na ukingo wa juu maarufu kama Notch kwaajili ya kuweka kamera na Sensor maalum, kampuni ya samsung yenyewe inatarajia kuja na muundo wa Galaxy S10 wa tofauti kabisa.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, Galaxy S10 inatarajiwa kuja na kamera ambazo zitakuwa juu ya kioo na sio kwenye ukingo wa juu kama ilivyo zoeleka kwenye simu nyingi za mwaka huu.
Mbali na hayo Galaxy S10 inatarajiwa kuja na sehemu ya Fingerprint ambayo iyakuwa chini ya kioo, kingine zaidi ni kuwa sehemu hii itakuja na teknolojia ya kisasa ya 3D ambayo itakuwa inafanya sehemu hiyo kufanya kazi kwa haraka zaidi. Vilevile inasemekana inawezekana kuwa Galaxy S10 kutokuwa na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, lakini usiwe na wasiwasi tetesi hizi hazina uhakika lakini ni vizuri kujua hili endapo litatokea.
Kwa upande wa Galaxy S10 Plus yenyewe inatarajiwa kuja na muundo wa tofauti zaidi huku ikiwa na kamera mbili kwa mbele pamoja na kamera nne kwa nyuma. Kwa mujibu wa tetesi mpya mtandaoni Galaxy S10 Plus inatarajiwa kuja na kamera hizo ambazo zinasemekana kufanya kazi sawa na simu ile ya Galaxy A9 iliyotoka miezi michache iliyopita.
Mfumo wa Uendeshaji
Kwa upande wa mfumo, Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus inatarajiwa kuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie) mfumo ambo juu yake unakuja na mfumo mpya wa Samsung wa OneUI ambao unakuja na muonekano wa icon mpya kabisa.
Vilevile mfumo huu mpya wa OneUI unatarajiwa kuja na sehemu mpya nyingi ikiwa pamoja na sehemu mpya ya Dark Mode ambayo itafanya simu hizi kuweza kudumu na chaji zaidi.
Mengineyo
Mbali na yote Galaxy S10 na S10 Plus zinasemekana kuja na processor zenye nguvu sana za Snapdragon 8150 au Exynos 9820 ambazo unaweza kupata kati ya hizo kutokana na nchi ambayo utanunua simu hiyo. Vilevile inasemkana kwamba etii kutakuwa na toleo jipya la simu hizi lenye uwezo wa mtandao wa 5G na pia toleo hilo litakuwa na RAM kubwa zaidi… sisi hatuna uhakika sana na hili lakini pengine tusubiri Mungu akituvusha salama tutaweza kuona.
Na hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kujua kuhusu tetesi za Galaxy S10 na S10+, Kwa habari zaidi za simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
kaka pongezi kwa kazi nzuri namna hii tuko pamoja sana mimi nikiwa kama mdau mkubwa wa hivi vitu