Habari na karibu tena Tanzania Tech, natumaini wote mko salama na mmesherekea vyema siku ya Christmas kwa kuangalia Movie nzuri nilizo kuhabairisha siku ya jana, vipi umeonaje movies hizo kama ulifanikiwa kuangalia unaweza kutuhabairisha kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
Anyway kwa siku ya leo nimekuandalia makala ambayo ukweli imenichukua muda mrefu sana kuandaa, na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na sababu ya simu nyingi kuwa bora sana mwaka huu 2018. Anyway baada ya kuangalia kwa makini na kusoma makala mbalimbali nimefanikiwa kupanga list ya simu 5 ambazo kwa upande wangu nahisi ni simu bora za mwaka 2018.
Kumbuka list hii ni kwa mujibu wa mimi na timu ya Tanzania Tech kwa ujumla hivyo inawezekana kwa upande wako ukaona tofauti kulingana na mahitaji yako au kulingana na unachoangalia kwenye simu husika. Kwa upande wetu kwenye list hii tumeangalia mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kamera, uwezo wa simu yenyewe pamoja na muundo kwa ujumla. Basi bila kupoteza muda mrefu basi twende tukangalie list hii.
5. Apple iPhone XR
Kama list ya simu hizi ingekuwa na namba zaidi ya namba 5 basi simu hii ingekuwa simu ya 10 kwenye list hii. Apple iPhone XR ni moja kati ya simu zinazo semekana kuwa za bei rahisi za mwaka huu kutoka kampuni ya Apple, lakini japokuwa simu hii ni ya bei nafuu bado inakuja na sifa nzuri sana kiasi kwamba simu hizi zilipo toka tu zilinunuliwa zote zikaisha kwa baadhi ya maduka nchini marekani. Tofauti ya iPhone XR na simu nyingine za Apple mwaka huu ni aina ya kioo tu lakini kwa upande wa sifa simu hii iko sawa na iPhone nyingine za mwaka huu 2018.
4. Google Pixel 3
Google Pixel ni moja kati ya simu nzuri sana kwa mwaka 2018 uzuri wa simu hizi hauishi kwenye muonekano wake bali pia uwezo wa simu hii. Google Pixel 3 ni moja kati ya simu ambayo inakuja na kamera nzuri sana. Mbali na hayo simu hii inauwezo mzuri wa sifa pamoja na uwezo mzuri wa kudumu na chaji, kifupi ni kwamba kama unataka simu yenye kila kitu unacho hitaji basi Google Pixel ni simu bora sana kwako.
3. Apple iPhone XS Max
Apple iPhone XS Max ni simu nyingine kutoka kampuni ya Apple ambayo imeingia kwenye list hii ya simu bora za mwaka 2018. Ukweli ni kwamba kama unatafuta simu yenye uwezo wa kufanya mambo kwa uhakika basi iPhone XS Max ni simu bora sana ya kuwa nayo. Simu hii inakuja na sifa nzuri sana pamoja na kamera bora na kama wewe ni mtumiaji wa simu za iPhone basi lazima unajua bora wa kamera za iPhone hivyo sidhani kama nahitaji kuongea sana kwenye hili.
2. OnePlus 6T
OnePlus ni moja kati ya kampuni changa za utengenezaji wa simu hivi sasa, kampuni hii ilizaliwa mwaka 2013 lakini mwaka 2018 kampuni ya hiyo imeweza kuteka soko la Smartphone kwa simu yake ya OnePlus 6T, ambayo imekuwa simu ya pili bora zaidi kwa mwaka 2018. Simu hii imekuwa bora kutokana na sifa zake nzuri na pia simu inapatikana kwa bei nafuu zaidi. Simu hii ukweli inakidhi kila haja ya mtumiaji wa simu hivyo kwa heshima na taathima ukweli OnePlus 6T ina kila haki ya kuwepo namba 2 kwenye list hii.
1. Samsung Galaxy Note 9
Samsung kwa mara nyingine tena wameweza kushilia chati kwa kuwa na simu bora kwa mwaka 2018. Kama wewe ni mmoja wa watu wanao hitaji simu basi napenda kukwambia Galaxy Note 9 its one of the best Smartphone in 2018. Simu hii inakuja na sifa nzuri sana, inakuja na kamera nzuri na pia inakuja na muundo mzuri sana, simu hii imeshikilia chati hii kutokana na ubora huo pamoja na uwezo wake wa kufanya kazi kwa ujumla. Ukweli nimetumia simu hii kwa siku kadhaa na matokeo yake ni mazuri sana hadi asilimia 99.
Anyway, hizi ndio simu bora kwa mwaka 2018. Chati hii inafunga ukurasa wa simu bora kwa mwaka huu 2018 na pengine Mwenyezi Mungu akipenda tukutane tena mwaka 2019 kwaajili ya kuanza kutazamia simu nyingine bora zitakazo kuja kwa mwaka huo 2019.
Kwa sasa hii ndio list yetu hapa Tanzania Tech lakini najua na wewe una list yako ya simu bora kwa mwaka 2018, Tuambie kwenye maoni hapo chini je unakubaliana na sisi au pengine simu gani ina stahili kuwepo kwenye nafasi ya kwanza.? Tuambie kwenye maoni hapo chini.
Yaah list imesimama kabisa
Karibu sana.