Sifa Kamili Pamoja na Bei ya Simu Mpya ya Nokia 8.1

Zifahamu hapa hizi ndio sifa pamoja na bei ya simu mpya ya Nokia 8.1
Sifa pamoja na bei ya Nokia 8.1 Sifa pamoja na bei ya Nokia 8.1

Kampuni ya Nokia hapo jana ilifanikiwa kumaliza kufanya uzinduzi wake ambao ulitegemewa kuingiza sokoni simu mpya za Nokia ikiwemo simu mpya ya Nokia 8.1, Kama ilivyo weza kutabiriwa hatimaye Nokia jana ilizindua simu hiyo na ni kweli kuwa simu hii ni toleo la kimataifa la simu ya Nokia X7 (2018) ambayo ilizinduliwa miezi michache iliyopita huko nchini China.

Kama ilivyo Nokia X7, Nokia 8.1 pia inakuja na kioo cha inch 6.18” PureDisplay IPS LCD ambacho kinakuja na resolution ya 1080p+ pamoja na ukingo wa juu. Ukingo huo wa juu unahifadhi kamera ya mbele ya Megapixel 20 pamoja na sensor mbalimbali. Pia kupitia settings za ndani ya simu hii utakuwa na uwezo wa kuzima ukingo huo wa juu.

Advertisement

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili za Megapixel 12 na 13 ambazo hizi zinakuja na teknolojia ya AI. Kamera moja ya Megapixel 13 hii depth sensor ambayo pia inasaidiwa na MP 12 ambayo hii inakuja na teknolojia ya Optical Image Stabilization.

Nokia 8.1 inaendeshwa na processor ya Snapdragon 710 chipset inayo saidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64. Unaweza kuongeza ukubwa huo wa ndani kwa kutumia Memory card hadi ya GB 400, Sifa nyingine za Nokia 8.1 ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 8.1

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~408 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie), yenye Android One
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.0, 0.9µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye Huku zote zikiwa zinasadiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3200 mAh battery battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa nne za Dark Blue, Night Red, Magic Night Silver, Night Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Tofauti kubwa iliyopo kwenye simu hii mpya ya Nokia 8.1 na Nokia X7 (2018) ni aina ya mfumo wa uendeshaji ambapo Nokia 8.1 inakuja na mfumo wa Android 9.0 (Pie) mfumo ambao ni mfumo wa Android One. Nokia X7 (2018) yenyewe inakuja na mfumo wa Android 8.1 Oreo lakini pia unaweza ku-update kwenye kwenye mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie).

Kitu kingine cha tofauti ni kwenye ukubwa wa ndani, Nokia 8.1 inakuja kwa toleo moja tu ambalo linakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 pekee, Nokia X7 (2018) yenyewe inakuja na matoleo mawili ya ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 128. Mbali na hayo sifa nyingine za simu hii zinafanana kila kitu.

Bei ya Nokia 8.1

Nokia 8.1 inatarajiwa kuanza kupatikana kwanza kwenye nchi United Arab Emirates na bei yake inatarajiwa kuanzia Dirham AED 1,500 ambayo hii ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 940,000 na Shilingi za Kenya Ksh 42,000. Kumbuka bei hii haijajumlishiwa na kodi hivyo bei inaweza kuongezeka au kupungua kutokana na Kodi. Oda za simu hii zinategemewa kuanza kupokelewa kuanzia siku ya leo huku upatikanaji ukitegemewa kuanzia tarehe 20 mwezi huu desemba soma zaidi kuhusu upatikanaji wa simu hii hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use