Zifahamu Hapa Sifa na Bei ya Huawei P Smart (2019)

Hii ndio simu mpya ya Huawei P Smart ya Mwaka 2019
Zifahamu Hapa Sifa na Bei ya Huawei P Smart (2019) Zifahamu Hapa Sifa na Bei ya Huawei P Smart (2019)

Kampuni ya Huawei hivi leo imetangaza kuanza rasmi kupokea oda za simu yake mpya ya Huawei P Smart (2019) na ifikapo mwezi january mwaka ujao 2019 simu hizo zitaanza kupatikana rasmi. Simu hii inakuja na kioo cha Inch 6.21 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080×2340 pixel.

Huawei P Smart (2019) inaendeshwa na processor ya Hisilicon Kirin 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card hadi ya GB 512. Mbali na hayo simu hii inakuja na battery ya 3,400mAh ambayo inaweza kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi yako, sifa nyingine za Huawei P Smart ni kama zifuatazo.

Sifa na bei ya Huawei P Smart (2019)
Huawei P Smart (2019)

Sifa za Huawei P Smart (2019)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2340 pixels (~415 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
  • Aina ya Processor – Hisilicon Kirin 710 (12 nm)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (HDR, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 (f/1.8) na Kamera nyingine inayo Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3400 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black za Aurora Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity na compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Huawei P Smart (2019)

Kwa upande wa bei, Huawei P Smart (2019) inatarajiwa kupatikana kuanzia Euro €250 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 660,000 bila kodi. Simu hii inategemea kuanza kupatikana kuanzia tarehe 2 ya mwezi january mwaka 2019.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use