Niwazi kuwa binadamu tunaendeshwa na historia ndio maana ni muhimu sana kwetu kukujuza mambo mbalimbali ya historia hasa yanayohusu teknolojia, pengine hii inaweza kuwa nafasi yako ya kujifunza tulipo toka kwa namna moja ama nyingine au pengine inaweza ku-kufundisha mengi zaidi kuhusu uvumilivu au kukuburudisha kwa namna yoyote.
Kwa kusema hayo leo kwenye makala hii nimekuandalia mambo 6 ya kihistoria kwenye upande wa teknolojia ambayo huenda kwa namna moja ama nyingine ulikuwa huyajui. Long story short, Najua hupendi kusoma makala ndefu hivyo basi twende moja kwa moja kwenye mambo haya.
TABLE OF CONTENTS
- 1 Kampuni za HP, Google, Microsoft na Apple zote Zilianzia Karakana (Garage)
- 2 Barua Pepe (Email) iligunduliwa Mapema Hata Kabla ya Internet
- 3 Hard Disk ya GB 1 ilikuwa ikiuzwa kwa Dollar za Marekani $40,000 sawa na Tsh Milioni 92
- 4 Michael Jackson alifariki Saa 3:15pm, Muda huo Mitandao ya Twitter, Wikipedia, na AOL IM Ilishindwa Kufanya Kazi.
- 5 Website ya Kwanza Kabisa Duniani ni info.cern.ch
- 6 Headphone za Kwanza Ziligunduliwa Jikoni
Kampuni za HP, Google, Microsoft na Apple zote Zilianzia Karakana (Garage)
Kampuni ya HP ilizaliwa mwaka 1938 huko Addison Avenue in Palo Alto, California nchini marekani. HP ilizaliwa kwenye karakana ambayo David Packard na Bill Hewlett wilianzisha mara baada ya kupewa wazo na Professor wao wa chuo ambaye aliwashauri wanafunzi wake kuanzisha makampuni yao ya kiteknolojia kwenye eneo hilo. Ina aminika kuwa David Packard na Bill Hewlett ndio wa kwanza kufanyia kazi mawazo hayo na ndipo walipo anzisha kampuni hiyo ya HP ambayo imebeba maana ya majina yao yani Hewlett Packard.
Kwa mujibu wa tovuti ya CNBC, Google ilianzishwa rasmi mwaka 1998 waanzilishi wa kampuni hiyo ya Google walikuwa Larry Page na Sergey Brin ambao walikodisha karakana (Garage) kwa ajili ya ofisi yao ya kwanza kutoka kwenye nyumba ya Susan Wojcicki ambaye sasa ndie kiongozi wa mtandao wa YouTube.
Microsoft yenyewe ilianzishwa mwaka 1975, kwenye karakana Garage iliyo kuwa inamilikiwa na Bill Gates. Karakana hiyo ilikuwa ndogo sana na ilikuwa na vyumba vya watu wawili cha Bill Gates na rafiki yake Paul Allen wote walianzisha kampuni hiyo ambayo ilikuwa inaitwa Micro-Soft.
Kwa upande wa Apple nayo ilianzishwa mwaka 1976 kwenye karakana ambapo walikuwa watu wawili Steve Jobs na Steve Wozniak.
Barua Pepe (Email) iligunduliwa Mapema Hata Kabla ya Internet
Inasemekana barua pepe ya kwanza inapatika kwenye kampyuta za MIT ambapo ilituma mwaka 1965. Kipindi hicho watumiaji wa kompyuta za MIT walikuwa wanauwezo wa kutumiana ujumbe ambao huu ulikuwa unaonekana endapo tu mtumiaji atakuwa anawasha kompyuta yake.
Mwaka 1969, Wizara ya ulinzi ya marekani ilitengeneza mfumo unaoitwa ARPANET (Advanced Research Projects Agency Network), mfumo ambao ulikuwa unaziunganisha kompyuta za wizara hiyo kwa ajili ya kuwasiliana ndani ya wizara hiyo. Tarehe 29 October mwaka 1969 barua pepe ya kwanza ilitumwa kupitia mfumo wa ARPANET. Inasemekana mwaka 1971 Ray Tomlinson ndie aliye gundua mfumo wa kutuma barua pepe wa kielektroniki, mfumo ambao unatumika kutuma barua pepe hadi sasa.
Hard Disk ya GB 1 ilikuwa ikiuzwa kwa Dollar za Marekani $40,000 sawa na Tsh Milioni 92
Hapo mwaka 1980, kampuni ya IBM ilifanikiwa kutengeneza Hard Disk iliyokuwa na uwezo wa GB 1 na inasemekana ilikuwa na ukubwa wa size ya kinanda na ilikuwa ikiuzwa kwa dollar 40,000 ambayo kwa sasa ni zaidi ya Milioni 92 za kitanzania.
Michael Jackson alifariki Saa 3:15pm, Muda huo Mitandao ya Twitter, Wikipedia, na AOL IM Ilishindwa Kufanya Kazi.
Kwa mujibu wa Wikipedia, inasemakana mtandao wa Twitter ulishindwa kufanya kazi kutokana na watu ku-tweet Tweet nyingi zaidi (asilimia 15 ya tweet zote) huku wakitaja jina la Michael jackson. Mtandao wa Wikipedia ulishindwa kufanya kazi kutokana na watu wengi zaidi kwa sekunde kusoma wasifu wa Michael Jackson kwa pamoja, pia inasemakana mtandao wa AOL nao ulishindwa kufanyakazi kwa zaidi ya dakika 40.
Website ya Kwanza Kabisa Duniani ni info.cern.ch
Tovuti ya kwanza kabisa duniani ilichapishwa tarehe 6 mwezi wa nane mwaka 1991 na mwingereza aliyekuwa anae julikana kama Tim Berners Lee. Tovuti hiyo ilichapishwa ikiwa na lengo la kujulisha ulimwengu kuhusu project mpya ya World Wide Web, tovuti hiyo iliachapishwa kwa kutumia kompyuta ya NEXT katika Shirika la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia, CERN. Unaweza kusoma ukurasa huo wa kwanza hapa.
Headphone za Kwanza Ziligunduliwa Jikoni
Kwa mujibu wa tovuti ya Stuff, Mwaka 1910 mhandisi Nathaniel Baldwin aligundua headphone za kwanza akiwa kwenye meza ya jikoni kwake. Wazo lake hilo haliku kukubalika na wawekezaji wa kawaida na hatimaye baadae jeshi la majini la marekani (US Navy) lilihitaji headphone 100 kutoka kwa mhandisi huyo na kwa mujibu wa Stuff jamaa huyo alitajirika sana kutokana na fedha hizo. Lakini Inasemekana baadae Nathaniel Baldwin alifilisika.
Na hayo ndio mambo sita ambayo nimekuandalia kwa siku ya leo, kama unataka makala zaidi za Je wajua unaweza kusoma makala zetu nyingine hapa. Kwa habari zaidi za Teknolojia hakikisha unaendelea kutembela Tanzania Tech kila siku.