in

Apps #24 App za Kuongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android

Jaribu app hizi nzuri za kuongeza ulinzi kwenye simu ya Android

Apps #24 App za Kuongeza Ulinzi Kwenye Simu ya Android

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android na kwa namna moja ama nyingine ungependa kuimarisha ulinzi wa simu yako basi unasoma makala sahihi. Kupitia kwenye sehemu ya 24 ya makala hizi leo tunaenda kuwaletea apps nyingine nzuri za android ambazo zinaenda kusaidia kuongeza ulinzi wa simu yako kwa kiwango kikubwa sana.

Apps hizi zote zinapatikana kupitia soko la Play Store hivyo kama unataka app yoyote kwenye list hii unaweza kubofya kwenye link maalum ya app hiyo na utapelekwa Play Store kwaajili ya kudownload app usika. Basi kwa kusema hayo twende moja kwa moja tukangalie app hizi.

Calculator Vault

Calculator vault ni app nzuri sana ya Android ambayo hii inakusaidia kuficha picha mbalimbali kwenye Gallery ya simu yako. App hii inaonekana kama caliculator na inafanya hesabu kabisa ikiwa unataka kufungua picha ulizoficha basi utaweka hesabu fulani ambayo wewe ndio utakuwa unajua na sehemu nyingine ya Gallery itafunguka ikiwa na picha zako ulizoficha. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia app hii.

Intruder Selfie

Intruder Selfie™
Price: Free

Kama kwa namna yoyote ukiacha simu yako mahali kuna mtu anaishika alafu ukiuliza anakataa basi app hii itakusaidia sana kuweza kujua anaeshika simu yako. App hii inauwezo wa kutuma picha ya mtu anaeshika simu yako mara kwa mara hata yule aliyeshika kwa mara moja tu akitaka kufungua simu yako. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia app hii.

Jaribu App Mpya ya Tanzania Tech Lite

Private SMS and Call

Kama kwa namna yoyote ungependa kuficha SMS pamoja na historia ya kupiga au kupigiwa simu basi app ya Private SMS and Call ni App nzuri kwako. App hii itakusaidia kuficha kabisa meseji ambazo hupendi zionekane pia itakusaidia kuweza kuficha Call Logs zako. Unaweza kujifunza jinsi ya kutumia App hii hapa.

Recycle Master

Kama unajua simu yako ina mtindo wa kushikwa na mtu zaidi ya mmoja na mtu huyo anaweza kufuta kitu kwenye simu yako kwa bahati mbaya basi unahitaji app hii ya Recycle Master. App hii itakusaidia pale unapofuta kitu kisipotehe moja kwa moja kwani sasa kila kitu utakachokuwa unafuta kitahifadhi kwenye app hii kabla ya kufutwa kabisa kutoka kwenye simu yako.

Unseen

Unseen - No Last Seen
Price: Free+

Unseen ni app nzuri sana kama unataka kusoma meseji zako za mitandao kama Facebook Messenger, WhatsApp, Instagram, Viber, Telegram, KakaoTalk, Line, Imo na VK bila mtu kujua kama uko hewani na bila mtu kujua kama umesoma meseji hiyo. App hii inauwezo mzuri sana wa kuficha Last Seen na pia una uwezo wa kusoma meseji za mitandao hiyo bila mtu kuona kama umesoma meseji hiyo.

Apps Nzuri za Kuangalia Mpira Kupitia Simu ya Android

WhatsRemoved+

WhatsRemoved+
Price: Free+

WhatsRemoved+ ni app nzuri sana ambayo inaweza kukusaidia kusoma meseji mbalimbali za WhatsApp ambazo mtu alikutumia alafu akafuta ili usiweze kusoma. App hii inauwezo wa kufanya kazi kwenye app zote za WhatsApp kwa pamoja yani WhatsApp Business pamoja na WhatsApp ya kawaida.

Hide App

Kama kwa namna yoyote kwenye simu yako unazo apps ambazo hutaki watu wajue kama zipo kwenye simu yako basi jaribu app hii ya Hide App. App hii inauwezo wa kuficha app zako mbalimbali kwa haraka na kwa urahisi zaidi, App utakazo ficha zitapotea kabisa kwenye kioo cha simu yako hivyo huna wasiwasi wa mtu kuweza kuona app hiyo.

Na hizo ndio app nzuri nilizo kuandalia kwa simu ya leo, kama una taka kujua apps nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android unaweza kusoma makala yetu uliyopita kupitia hapa.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.