Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Simu Mpya za Samsung Galaxy A8s na Galaxy M

Simu hizi zitakuwa za kwanza kuja na vioo visivyo na ukingo ( Infinity O display )
Simu mpua za Galaxy A8s na Galaxy M Simu mpua za Galaxy A8s na Galaxy M

Siku za karibuni Samsung kupitia mkurugenzi mtendaji wake Dj koh ilitangaza kuwa sasa inaenda kubadilisha mtazamo wa kampuni hiyo na kuangalia zaidi simu za kiwango cha kati kuliko zile simu za kiwango cha juu. Dj Koh alisema kuwa Samsung inategemea kuleta sehemu mpya zaidi kwenye simu za kiwango cha kati zaidi kuliko zile za kiwango cha juu tofauti na ilivyo zoeleka.

Sasa naposema simu za kiwango cha kati hapa na maanisha zile simu ambazo sio za bei ghali sana na sio za bei rahisi, yani ziko katikati. Mfano wa simu hizi ni kama Galaxy A8, Galaxy A8 Star, Galaxy A9 au A7 na simu nyingine nyingi, pia vile vile napozungumzia simu za viwango vya juu au daraja la juu hapa namanisha zile simu za Galaxy S9 na Galaxy Note 9 na nyingine kama hizo.

Advertisement

Sasa katika kuanza kutekeleza hazma hiyo, hivi karibuni kampuni ya Samsung inatarajia kuja na simu mpya mbili za Galaxy A8s pamoja na matoleo mapya ya simu za Galaxy M. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali Galaxy A8s itakuwa ni simu ya kwanza ya daraja la kati kuja na mtindo mpya wa kioo ambacho kitakuwa hakina ukingo kabisa au kwa kitaalamu Infinity O display.

Mfano wa Galaxy A8s
Mfano wa Galaxy A8s

Mbali na hayo simu hii ya daraja la kati pia itakuwa ni miongoni mwa simu za awali ambazo zitakuwa na kamera ya mbele ambayo iko ndani ya kioo kama inavyo onekana kwenye picha za mfano hapo juu. Hata hivyo inasemekana Galaxy A8s itakuja na processor ya Snapdragon 710 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6. Simu hii pia inasemekana kuja na battery ya 3,000 mAh battery ambayo inasemekna kuja na uwezo wa fast charging.

Tetesi zinasema kuwa simu hii inatarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2019, huku watu wengine pia wakidai simu hii inaweza kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka huu 2018. Yote ya yote endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza kila kitu kuhusu simu hii.

Matoleo Mapya ya Samsung Galaxy M

Sasa tukija kwa upande wa Galaxy M, simu hizi zinasemekana kuja na matoleo mengi zaidi na pia inasemekana simu hizi zitakuwa ni simu za bei rahisi kidogo. Kwa mujibu wa habari mpya hivi karibuni, Kampuni ya Samsung inatarajia kuuza simu hizi zaidi kwenye nchi za Afrika, Mashariki ya kati pamoja na Asia. Vilevile simu hizi zinatarajiwa kuja na uwezo mzuri sana ikiwa pamoja na ukubwa wa ndani wa hadi GB 128.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu simu hii, ila ripoti za hivi karibuni zinadai kuwa kupitia simu hizi Samsung itabadilisha mtindo wa majina yake kwenye simu na sasa itakuwa inatumia namba mbili tofauti na hapo awali. Kwa mfano Galaxy A8s inatarajiwa kuja na matoleo kama A50 na A30, vilevile Galaxy M nayo inatarajiwa kuja na matoleo mengine kama M10, M20 pamoja na M30 huku ikisemekana simu hizo kuja na ukubwa wa ndani kama inavyoelekeza hapo chini.

Kwa sasa bado hakuna tarehe kamili ya kutoka kwa simu hizi na pia inasemekana bado kampuni hiyo haijaanza rasmi kutengeneza kwa wingi simu hizi hivyo huwenda ukubwa wa ndani ulioweza kuona hapo juu ukabadilika kwa kuongezeka au kwa kupungua. Kwa taarifa kamili kuhusu simu hizi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use