Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video : Hii Hapa Simu ya Kwanza ya Samsung Inayo Jikunja

Hivi karibuni Samsung imeonyesha simu yake inayo jikunja
simu ya samsung inayo jikunja simu ya samsung inayo jikunja

Simu za kujikunja au Foldable phone ziko mbioni kuja kwa watumiaji wa simu za mkononi, iwe wewe ni mpenzi wa simu hizo au lah lakini ukweli ni kwamba simu hizo zinakuja hivi karibuni. Hii imedhirika kutokana na kampuni nyingi za simu kuwa na kasi ya kuonyesha simu hizo zinazojikunja.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech lazima utakuwa unajua kuwa hivi karibuni kampuni moja ya nchini China inayoitwa Royole ilizindua simu inayo jikunja inayoitwa FlexPai, simu hii sio ya kwanza kutengenezwa kwa mtindo huu, bali ni simu ya kwanza kabisa kutengenezwa kwa mtindo huo na kufanikiwa kuingia sokoni na kuuzwa kwa wateja mbalimbali.

Advertisement

Sasa mbali ya FlexPai, hapo juzi kampuni ya Samsung nayo kwa mara ya kwanza imeonyesha simu yake ya kwanza ambayo inajikunja. Simu hiyo iliyoonyeshwa kwenye mkutano wa Samsung Developer Conference mkutano ambao unafanyika kila mwaka na ukihusisha wabunifu wa programu na teknolojia mbalimbali. Sasa kama hukufanikiwa kuona video hiyo nimekuwekea kipande kifupi cha video hiyo hapo chini.

Kama nilivyo kwambia hapo awali hiyo ni video fupi tu kwani Samsung haikuonyesha simu hiyo kwa muda mrefu kwa madai kuwa simu hiyo bado haijakamilika ndio maana umeona kwenye video huyo taa zilizimwa kidogo ili kuficha muundo kamili wa simu hiyo.

Lakini pamoja na hayo mpaka kufikia hapo ina maana kuwa kampuni ya Samsung iko kwenye hatua nzuri sana ya kuleta simu hiyo kwa wateja wake siku za karibuni, lakini mbali ya Samsung ziko kampuni nyingine kama Huawei, LG, Xiaomi, Oppo, Lenovo na Motorola ambazo nazo ziko kwenye hatua ya kutengeneza simu zake ambazo zina jikunja (Foldable Phone).

Lakini pia kama haitoshi, Google nayo kupitia mfumo wa Android imetangaza mabadiliko ambayo yatakuja siku za karibuni ambayo yatakuwa zaidi kwenye tovuti na app mbalimbali za Google ikiwa pamoja na YouTube. Sasa kama wewe utakuwa mmoja wa watu ambao watakuwa wanatumia simu za aina hii yaani simu zinazo jikunja, utaweza kufurahia kuangalia video kwenye mtandao wa YouTube iwe umefungua simu yako au umefunga simu yako.

Video : Hii Hapa Simu ya Kwanza ya Samsung Inayo Jikunja

Mbali na hayo, pia Samsung imetangaza kuja na mfumo mpya wa One UI mfumo ambao unakuwezesha kutumia simu ya aina hii kwa urahisi na haraka. Kwa mujibu wa samsung, mfumo wa One UI unategemewa kuleta aina tofauti kabisa za namna unavyo tumia simu yako ikiwa pamoja na njia rahisi za kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hasa unapokuwa na simu hizi zina zojikunja.

Kwa sasa bado hakuna tarehe kamili ya lini simu hii ya Samsung itaingia sokoni, lakini ni uhakika kuwa tegemewa kuona simu hii kwenye mkutano wa CES 2019 ambao hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili.

Bila shaka hadi hapo umejua kuwa simu hizi zinazo jikunja zinakuja siku za karibuni hivyo ni vyema kuwa tayari kupokea teknolojia hii ambayo ukweli itabadilisha sana jinis ambavyo simu za kawaida zinavyotumika. Vipi uko tayari kwa simu zinazo jikunja tuambie kwenye maoni hapo chini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use