Kampuni ya Tecno inajiandaa kuja na simu mpya ya Tecno Camon 11, Simu ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi hapo siku ya jumatatu ya tarehe 12 mwezi huu November. Mbali ya hayo simu hii itakuwa ya kwanza kutoka kampuni ya Tecno kuja na ukingo wa juu maarufu kama Top Notch.
Kama utakuwa ni msomaji wa tovuti hii ya Tanzania Tech lazima utakuwa umesha wahi kuona picha hiyo hapo juu kwani hiyo ni Tecno iClick 2, simu mpya ya Tecno iliyozinduliwa huko nchini India.
Simu hii mpya ya Tecno Camon 11 inatarajiwa kuja na teknolojia ya AI kwenye kamera zake hivyo inategemewa kuwa kamera hizo zitakuja zikiwa na zinapiga picha vizuri zaidi. Mbali na hayo simu hii ya Tecno Camon 11 inategemewa kuja na toleo lingine la Tecno iClick 2 Pro, toleo ambalo litakuwa na ukubwa wa ndani mkubwa zaidi na RAM kubwa zaidi.
Kwa sifa za awali simu hii inatarajiwa kuja na kioo cha inch 6.1 mfumo wa uendeshaji wa Android Oreo 8.1, Processor ya MediaTek Helio A22 processor ambayo inasaidiwa na RAM ya 3 au GB 4 kwa toleo la Camon 11. Simu hizi zinasemekana kuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 kwa toleo la kawaida na ukubwa wa GB 64 kwa toleo la Camon 11 Pro.
Kwa upande wa kamera, Camon 11 na Camon 11 Pro zinategemewa kuja na kamera mbili kwa nyuma huku toleo la kawaida likiwa na kamera za Megapixel 13 na Megapixel 5, na toleo la Pro likitarajiwa kuja na kamera za Megapixel 16 na Megapixel 5 pamoja na kamera ya mbele ambayo yenyewe itakuwa na Megapixel 24 na Megapixel 16 kwa kamera ya mbele ya toleo la kawaida.
Kwa sasa Tayari simu hizi zimeshatoka rasmi hivyo unaweza kujua sifa kamili za Tecno Camon 11 na Tecno Camon 11 Pro kwa kusoma makala hapa.