Kampuni ya OnePlus ni moja kati ya kampuni zinazoongoza sana kwa utengenezaji wa simu bora mwaka 2018, mbali ya kuwa kampuni bora nchini India, Kampuni ya OnePlus inatengeneza simu zenye muonekano mzuri sana na ambazo zinapatikana kwa bei nafuu.
Sasa siku za karibuni, kampuni ya OnePlus imekuja na ingizo jipya ambalo ni toleo jipya la simu ya OnePlus 6, simu ambayo imezinduliwa miezi kadhaa iliyopita. Sasa toleo hili jipya la simu ambayo inaitwa OnePlus 6T, inakuja na kioo cha inch 6.4 ambacho kina ukingo wa juu maarufu kama notch, kioo ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya Optic AMOLED.
Mbali na hayo kioo hicho pia kinakuja na sehemu ya fingerprint ambayo hii iko chini ya kioo hicho ambacho kimetengenezwa kwa glass ngumu ya Corning Gorilla Glass 6, glass ambayo inafanya kioo hicho kuwa kigumu hasa pale simu hiyo inapo anguka.
Kwa upande wa sifa, OnePlus 6T inakuja na processor ya Snapdragon 845 chipset ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 8 au GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128 au GB 256. Kwa upande wa kamera, OnePlus 6T inakuja na kamera moja kwa mbele ambayo kamera hiyo inakuja na uwezo wa Megapixel 16, huku kwa nyuma ikiwa na kamera mbili za Megapixel 16 pamoja na nyingine yenye Megapixel 20 ambayo hii ni wide lens ambayo inasaidiwa na flash ya Dual-LED flash. Sifa nyingine za OnePlus 6T ni kama zifuatazo.
Sifa za OnePlus 6T
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.41 chenye teknolojia ya Optic AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, 19.5:9 ratio (~402 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
- Uwezo wa GPU – Adreno 630
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja itakuwa na GB 128 nyingine GB 256, zote zikiwa hazina sehemu ya kuweka Memory card.
- Ukubwa wa RAM – Machaguo mawili RAM ya GB 6 na nyingine itakuwa na RAM ya GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye (f/2.0, 20mm, 1/3″, 1.0µm), gyro-EIS, Auto HDR, 1080p.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko Mbili moja ina Megapixel 16 yenye uwezo wa (f/1.7, 27mm, 1/2.6″, 1.22µm, gyro-EIS, OIS) na nyingine yenye Megapixel 20 yenye (f/1.7, 1/2.8″, 1.0µm), kamera zote zina uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3700 mAh battery yenye uwezo wa Fast battery charging 5V 4A 20W (Dash Charge).
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE, aptX HD pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Mirror Black na Silk White.
- Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack, bali inakuja na USB maalum ambayo unaweza kuchomeka headphone jack.
- Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Mbele Chini ya Kioo).
Bei ya OnePlus 6T
Kwa upande wa bei simu hii inategemewa kuanza kupatikana kuanzia siku ya kesho tarehe 6 Novembar na inategemewa kuuzwa ka matoleo ya aina tatu. Toleo la kwanza litakuwa ni toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6 toleo ambalo litauzwa kwa dollar za marekani $550 ambayo ni sawa na Tsh 1,261,000 bila kodi. Toleo lingine ni toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 8 toleo hilo litauzwa kwa dollar za marekani $580 ambayo hii ni sawa na Tsh 1,329,000 bila kodi.
Toleo la mwisho litakuwa ni toleo lenye ukubwa wa ndani wa ndani wa GB 256 na RAM ya GB 8, toleo ambalo litauzwa kwa dollar za marekani $630 ambayo ni sawa na Tsh 1,444,000 bila kodi. Simu hizi zote zinategemewa kuanza kupatikana kwanza kwenye nchi za Amerika ya kaskazini, pamoja na ulaya. Kwa Tanzania bei ya simu hizi inaweza kuongezeka kutokana na kodi pamoja na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.