in

Kampuni ya Huawei Imekuja na Simu Mpya ya Honor 10 Lite

Zifahamu kwa undani hizi hapa ndio sifa za Honor 10 Lite

Sifa na Bei ya Honor 10 Lite

Hapo mwezi April mwaka huu 2018, kampuni ya Huawei kupitia kampuni yake ya Honor ilizindua toleo la simu ya Honor 10, toleo ambalo ilikuwa ni maboresho ya toleo la simu ya Honor 9 ya mwaka 2017.

Mwezi huu kampuni hiyo imerudi tena na Toleo jipya la simu ya Honor 10 Lite, Simu inayokuja na maboresho tofauti ya muonekano pamoja na sifa. Kwa mbele Honor 10 Lite inakuja na kioo cha inch 6.21 ambacho kwa juu kinakuja na ukingo mdogo ambao katikati yake kuna kamera ya kupiga picha za Selfie yenye uwezo wa Megapixel 24 ambayo pia inakuja na mfumo wa AI.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili ambapo kamera kuu inakuja na uwezo wa Megapixel 13 na kamera nyingine inakuja na Megapixel 2 ambayo yenyewe hii ni depth sensing lens. Honor 10 Lite inaendeshwa na processor ya Hisilicon Kirin 710 (12 nm) ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 4 na GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 128 na GB 64, ukubwa ambao unaweza kuongezwa kwa Memory Card yenye uwezo wa hadi GB 512.

Honor 10 Lite inapewa nguvu na Battery ya Li-Po yenye uwezo wa 3,400 mAh, Battery ambayo ikichajiwa vizuri inauwezo wa kudumu siku nzima kulingana na matumizi. Kujua zaidi sifa kamili za Honor 10 Lite ni kama zifuatazo.

Sifa za Honor 10 Lite

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2340 pixels (~415 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53)
  • Aina ya Processor – Hisilicon Kirin 710 (12 nm)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko kwa machaguo mawili GB 128 pamoja na GB 64 zenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko kwa machaguo mawili GB 6 na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 (f/1.8) na Kamera nyingine inayo Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3400 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Midnight Black, Lily White, Gradient Blue, na Gradient Red.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity na compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Honor 10 Lite

Kwa upande wa Bei, Honor 10 Lite inakuja kwa matoleo matatu, huku toleo la Honor 10 Lite yenye ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4 ikitarajiwa kuuzwa kwa Yuan ya China CNY1,399 ambayo ni sawa na Tsh 467,000 bila kodi, na toleo lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa GB 64 likitegemewa kuuza kwa Yuan CNY1,699 ambayo ni sawa na Tsh 567,000 bila kodi. Toleo la mwisho lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 kuuzwa kwa Yuan CNY1,899 ambayo ni sawa na Tsh 634,000 bila kodi.

Kwa sasa simu hizi zinategemewa kupatikana kupitia mtandao wa kuuza simu za Huawei nchini china, unao julikana kama Vmall.

Kampuni ya Huawei Imekuja na Simu Mpya ya Honor 10 Lite
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments