in

Zifahamu Hizi Hapa Programu za Kuflash Simu za Android

Tumia programu hizi kuflash simu za Samsung, Tecno, Infinix, iTel pamoja na Nokia

programu za kuflash simu

Imekuwa ni kitu cha kawaida sana siku hizi kwa watumiaji kuflash simu zao wenyewe, iwe ni kwa sababu ya kuondoa matatizo mbalimbali ya simu husika au kwa kufanya marekebisho fulani. Kuflash simu imekuwa sio tatizo la kupeleka simu yako kwa mtaalamu, Lakini japokuwa kuflash simu ni kitu cha kawaida na kirahisi lakini bado kuna tatizo juu ya upatikanaji wa programu za kuflash simu mbalimbali za Android.

Sasa kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tumekukusanyia programu maalum za kuflash simu ikiwa pamoja na link maalumu za kudownload programu hizo. Kumbuka, programu hizi zina tofautiana kwenye kila simu hivyo ni muhimu kusoma kwa umakini kabla uja download programu huzika.

Pia programu hizi za kuflash simu zina tofauti kwa matumizi hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafuata maelezo ya jinsi ya kutumia programu hizo kwa usahihi ili usije kuharibu simu yako. Pia ni muhimu kukumbuka kuflash simu yako kunaweza kuharibu baadhi ya mikataba kama vile warranty pamoja na mikataba mingine ya sehemu uliyo nunulia simu yako, hivyo kumbuka kuwa unafanya hivi kwa kutambua madhara ya kuflash simu yako.

Chat kwa Namna ya Kipekee kwa Kutumia Njia Hizi (Android)

Programu za Kuflash Simu

1. Odin – Samsung za Aina Zote

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Samsung, programu ya Odin ni muhimu wewe kuifahamu. Programu hii inauwezo wa kuflash tablet na simu mbalimbali za Samsung hata zile ambazo ni mpya kabisa kama vile Samsung Galaxy S9 na nyingine kama hizo. Programu hii ya kuflash simu haiuzwi na ni bure kabisa kutumia unachotakiwa ni kuwa na Firmware ya simu yako ya Samsung ambayo unaweza kuipata hapa, programu ya kuflash simu ya Odin unaweza kuidownload kupitia link hapo chini.

Download Odin Hapa

2. SP Flash Tool – Tecno, Infinix, iTel na Simu za China

Kama wewe ni mtumiaji wa simu za TECNO, Infinix na simu nyingine kama hizo ambazo zinatumia chipset ya MediaTek basi ni vyema kufahamu programu hii ya kuflash simu. Programu hii inaweza kuflash simu nyingi za kutoka nchini china na pia kama ilivyo programu ya kwanza kwenye list hii programu hii pia ni bure kabisa kudownload na pia ni bure kabisa kutumia, kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa na Firmware ya simu yako ambayo unaweza kuipata hapa. Kwa programu ya SP Flash tool unaweza kupakua kupitia link hapo chini.

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus

Download SP Flash Tool Hapa

3. Phoenix Suit – Nokia za Zamani

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu za Nokia za zamani basi ni vyema kufahamu programu hii ya Phoenix Suit, programu hii inauwezo wa kuflash simu mbalimbali lakini zaidi inauwezo wa kuflash simu za Nokia. Unaweza kuipata programu hii bure kabisa kupitia link hapo chini.

Download Phoenix Suit Hapa

Na hizo ndio programu za kuflash simu ambazo unaweza kuzitumia kuflash simu yako, programu hizi ni baadhi tu ambazo zimedhibitika kuweza kufanya kazi vizuri, kama kuna programu nyingine ambayo itajitokeza siku za karibuni basi moja kwa moja tutaiongeza hapa kwenye makala hii. Ili kuhakikisha hupitwi na habari yoyote hakikisha una download app ya Tanzania Tech.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.