Instagram imekuwa ni moja kati ya mtandao wa kijamii unaotumiwa sana siku hizi, kutokana na hilo, mtandao huo umekuwa ukifanyiwa mabadiliko mapya mara kwa mara. Sasa hivi karibuni kupitia tovuti ya habari ya Instagram, mtandao huo umeainisha kuanza kufanya majaribio ya Mabadiliko ya ukurasa wa Profile ndani ya mtandao huo.
Instagram imetangaza kuwa, mabadiliko hayo mapya yanayotegemewa kuanza siku za karibuni yatakuwa yanahusisha watu wachache ndani ya mtandao huo. Moja kati ya sehemu mpya kwenye mabadiliko hayo ni pamoja na sehemu mpya ya Store kwa kurasa za biashara, pamoja na sehemu mpya ya IGTV.
Kama unavyoona hapo juu, muonekano wa profile ni mpya kabisa huku picha ya profile sasa ikiwa inakaa kwa upande wa kulia. Mbali na hayo, Instagram pia imeandika kuwa inataka watumiaji wa mtandao huo kuangalia zaidi profile ya mtu kuliko followers, hivyo imefanya mabadiliko ya idadi ya namba za followers zinavyoonekana na sasa namba hizo zitakuwa chini ya jina tofauti kabisa na jinsi ilivyokuwa hapo mwanzo.
Instagram imeendelea kuandika kuwa, mabadiliko haya ni hatua za awali kwa sasa na mtandao huo utakuwa unapokea maoni ya watumiaji juu ya majaribio ya muonekano huo mpya. Instagram imesema kuwa majaribio haya hayato adhiri jinsi picha za watumiaji zinavyoonekana hivyo watumiaji hawana haja ya kuwa na wasiwasi.
Kwa sasa mtandao wa Instagram uko kwenye mchakato maalum wa kuondoa followers, like na comment feki ambazo zina kuwa zimepatikana kwa kutumia programu mbalimbali za kuongeza like, followers au Comment. Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu za namna hii nadhani ni wakati wa kuacha sasa kutumia programu hiyo kuepusha ukurasa wako kuweza kufutwa.