Kujua kama Simu Uliyonunua Dukani ni Mpya au Imetumika

Jinsi ya Kujua kama Simu Uliyonunua mpya au Refurbished
simu mpya zilizotumika simu mpya zilizotumika

Najua kichwa cha habari kime kushangaza kidogo, lakini ni kweli kwamba sio kwa sababu umenunua simu yako mpya dukani basi ni lazima kuwa wewe ndio mtu wa kwanza kutumia simu hiyo. Siku hizi kuna kampuni nyingi za simu uweza kutoa huduma nyingi ambazo humpa mteja nafasi ya kuweza kubadilisha simu yako uliyotumia na kuongeza hela kidogo na hatimaye kupewa toleo jipya la simu kutoka kampuni husika.

Sasa kutokana na hili simu nyingi sana zinazopatikana kutokana na huduma kama hizi hurudishwa kwenye soko kwa kuja kuuzwa barani afrika na nchi nyingine kwa bei ya punguzo. Kama ulikuwa unajiuliza, simu hizi huwezi kujua kwa macho hata kidogo. Kifupi ni kwamba hakuna kitu cha tofauti kwenye simu hizi kwani simu hizo zina kuja kwenye box na unaikuta na kila kitu chake.

Advertisement

Lakini pamoja na hayo, zipo baadhi ya njia ambazo unaweza kuzitumia kujua kama simu yako unayo tumia ni mpya au iliyotumika kwa lugha nyingine hizi huitwa refurbished phones. Sasa sio kwamba kampuni zinazo tengeneza simu hizi huficha kwamba simu hizo zimetumika na ndio maana kuna njia ambazo unaweza kutumia kujua kama simu unayotumia ni refurbished.

Jinsi ya Kujua Kama Simu ya iPhone Unayo Tumia Imetumika

Tukianza na iPhone njia hii ni rahisi na huitaji ku-install app yoyote kwenye simu yako, unacho hitaji kufanya ni kufanya hatua hizi. Fungua Sehemu ya Settings kisha Bofya General kisha Tafuta sehemu iliyo andikwa Model sehemu hii itakuwa inaanza na herufi na baadae kuwa na namba kama hivi “MN572LL/A”. Kama utakuwa umefika hapa fuata maelezo mengine hapo chini.

  1. Kama kwenye sehemu ya Model kumeanza na herufi M basi simu yako ulinunua ikiwa mpya kabisa.
  2. Kama kwenye sehemu ya Model kumeanza na herufi F basi simu yako ulinunua ikiwa imeshatumika.
  3. Kama kwenye sehemu ya Model kumeanza na herufi N basi simu yako ilibadilisha kutokana na ombi maalum kutoka kwa aliyekuwa anatumia.
  4. Kama kwenye sehemu ya Model kuanza na herufi P basi simu yako ilibadilisha baadhi ya vitu kutokana na ombi maalum la mteja.

Kwa kutumia njia hii utakuwa unaweza kujua kama simu yako ya iPhone ulinunua ikiwa imetumika au ikiwa mpya. Lakini kama unatumia simu ya Samsung basi unaweza kufuata njia hapo chini.

Jinsi ya Kujua Kama Simu ya Samsung ni Mpya au Imetumika

Kwa upande wa simu za Samsung unachotakiwa kufanya ni kudownload app ya Samsung iNFO kupitia soko la Play Store, Unaweza kupata app hii kwa kubofya link hapo chini.

Phone INFO ★SAM★

Baada ya kuinstall app hii kwenye simu yako sasa fungua app hiyo kisha bofya sehemu ya vimishale mitatu iliyoko juu upande wa kushoto, kisha chagua sehemu iliyoandikwa Refurbishment Check.

Baada ya kubofya hapo subiri kidogo kisha utaweza kuletewa meseji yenye ujumbe kama simu yako imeshawahi kutumika au ni mpya kabisa.

Kwa kutumia njia hii basi utaweza kujua kama simu yako ya Samsung imetumika au kama simu yako ni mpya kabisa. Kwa watumiaji wa simu nyingine za Android unaweza kutumia njia nyingine ambayo hii haifanyikazi kwa baadhi ya simu hivyo kama simu yako itakataa njia hii usishangae sana.

Sasa unachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yako kisha bofya namba hizi kwenye sehemu ya kupiga simu, bofya ##786# au *#*#786#*#* huna haja ya kubofya kitufe cha kupiga, kama Menu itatokea tafuta sehemu iliyo andikwa Reconditioned status kama kwenye sehemu hiyo kutakuwa na NO basi simu yako ni mpya kabisa, ila kama kutakuwa na YES basi simu yako ilishawahi kutumika.

Na hizo basi ndio njia ambazo unaweza kutambua kama simu yako ni mpya au imeshawahi kutumika kwa namna moja ama nyingine. Kumbuka sio kila mara simu zilizotumika zinakuwa na matatizo bali ni vyema kununua kitu ambacho wewe ndio wa kwanza kukitumia kwani tatizo lilifanya simu hiyo ikafunguliwa na kurekebishwa linaweza kurudi tena. Now you know..!

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use