Hatua za Jinsi ya Kuzuia Simu Kupata Moto Mara kwa Mara

Epuka haya kama unataka kuzuia simu yako kupata moto mara kwa mara
jinsi ya kuzuia simu kupata moto jinsi ya kuzuia simu kupata moto

Tatizo la simu kupata moto ni tatizo kubwa sana miongoni mwa watumiaji mbalimbali wa smartphone, ukweli ni kwamba kuna sababu nyingi sana zinazoweza kusababisha simu kupata moto na ndani ya sababu hizi zipo sababu nyingine ni za kawaida tu hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kila mara unapo sikia simu yako ina joto la kawaida.

Lakini kama simu yako imekuwa ikipata joto mara kwa mara tena hata kama hutumii simu hiyo basi ni wazi hilo ni tatizo kubwa na linahitaji kurekebishwa mara moja. Sasa zifuatazo ni hatua ambazo ukizichukua pengine unaweza kudhibiti tatizo hili lisiweze kutokea. Pia kama tatizo hili alijatokea kwenye simu yako basi nadhani ni wakati wa kuweza kufuata hatua hizi ili kuhakikisha tatizo hili halitokei kwa namna yoyote ile. Basi bila kupoteza muda let’s get to it..

Advertisement

1. Chaji Simu Yako na Chaja Sahihi

Jambo ambalo lina changia kwa asilimia 90 simu kupata moto ni pamoja na battery ya simu yako, ni muhimu kuhakikisha unazingatia usalama wa battery yako kwa kuchajia na chaji ambayo ni sahihi. Chaji sahihi ni ile ambayo inakuja na simu yako au ile ambayo inaendana na simu kwa namna zote ikiwa pamoja na kiasi cha umeme inachotoa.

Mara nyingi watu hutumia chaji tofauti na simu zao ili kuweza kuharakisha simu kujaa chaji au kwa sababu ya kutokua na chaji sahihi, lakini napenda kukwambia ni vyema kuacha kuchajia simu yako kwa hizo kwani chaji inayotoa umeme mdogo zaidi au mkubwa zaidi zote zinaweza kuharibu battery ya simu yako na kusababisha simu kuanza kupata moto sababu ya seli za battery kuchoka.

2. Chaji Simu Yako Kwa Usahihi

Ni kweli kwamba wengi wetu tunajua kuwa simu ikiisha chaji basi ni lazima kuweka kwenye chaji muda huo huo kwani hata hivyo ndio kazi ya simu yako, lakini ni vyema kuanza kutengeneza mpango wa kuchaji simu yako kwani battery ya simu kama ilivyo vitu vingine nayo pia ina muda wake wa mwisho wa matumizi, matumizi haya hufikia mwisho kwa haraka zaidi kulingana na jinsi unavyochaji simu yako mara kwa mara.

Sasa basi kama kuna ulazima ni vyema kuweka mpango wa kuchaji simu yako angalau mara mbili kwa siku, wakati wa mchana chaji simu yako hadi asilimia 50 na tumia mpaka usiku na uchaji mpaka iweze kujaa wakati wa usiku. Pia kumbuka kuvua kava la simu yako kwani hii inaweza kusababisha simu kupata joto pale inapochajiwa.

3. Kumbuka Kuzima Sehemu ya Location na WiFi

Application nyingi kwenye simu yako zina uwezo wa kuwasha sehemu ya location bila hata wewe kujua, kwa mfano app kama ya Uber inaweza kutumia sehemu ya location bila hata wewe kujua na endapo sehemu hii ikibaki ON kwa muda mrefu husababisha simu yako kupata joto sana.

Tatizo hili ni kubwa kwa watu wengi na pia ni moja ya sababu ya simu nyingi kuisha chaji kwa haraka zaidi. Hivyo basi hakikisha unazima WiFi na GPS kila mara unapo anza kuhisi simu yako inapata moto au kila mara baada ya kutumia app kama Uber na nyingine kama hizo.

4. Kumbuka Kupumzisha Simu Yako

Ni kweli kuwa hata simu yako inachoka kwa matumizi ya muda mrefu, hakikisha unapumzisha simu yako mara kwa mara baada ya kuitumia kwa muda mrefu hii ufanya processor ya simu yako kupoa na hivyo pia kufanya simu yako kupungua moto kwa haraka zaidi, pia hii husaidia battery kuweza kudumu na chaji kwa muda mrefu.

5. Zima Programu Zote Baada ya Kutumia

Moja kati ya sababu nyingine kubwa inayo sababisha simu kupata moto mara kwa mara ni pamoja na kuwa na programu ningi zinazofanya kazi kwa pamoja. Moja ya tatizo ambalo nimekutana nalo kwa watu wengi ni kuwa na magroup mengi yenye notification ambazo hazijasomwa, hii inatokana na kuwa pale notification zinapobaki juu bila kusomwa hufanya processor ya simu yako kuendelea kufanya kazi kwa kuonyesha hizo notification.

Kama una magroup mengi sana na huwezi kusoma mpaka muda fulani unaweza kutumia app ya Noti Save hii inaweza kusaidia kuhifadhi Notification kwa ajili ya kuzisoma baadae.

6. Ondoa File za Cache Mara kwa Mara

Cache ni file ambazo huifadhiwa kwenye simu yako ili kuweka kumbukumbu ya matumizi ya baadhi ya programu zako, Cache husaidia programu au App kufunguka haraka na hivyo file hizi ni muhimu pale unapotumia programu yoyote ndani ya simu yako. Lakini file hizi zinapozidi kwenye simu yako huweza kusababisha simu kustak, kuwa slow na pia kupata moto kwa haraka, hivyo basi hakikisha unafuta au una Clear Cache mara baada ya kuona simu yako inakuwa slow au inapata moto mara kwa mara.

7. Usiweka Kava Lenye Kuziba Kabisa Simu Yako

Tatizo lingine linalo sababisha simu kupata moto ni pamoja na kuweka kava ambalo linafunga kabisa simu yako. Kwa kawaida simu yoyote imetengenezwa kwa mtindo maalum ambao unaweza kusaidia simu kupunguza joto yenyewe, lakini tatizo linakuja pale unapokuwa umeweka Kava ambalo limejifunga kiasi cha kuweza kuchagia simu kupata joto zaidi. Kifupi unachotakiwa kufanya ni kutoa kava mara kwa mara unapokuwa utumii simu yako hii itasaidia simu kupunguza joto kwa kiasi kikubwa sana na hii itaongeza ufanisi wa simu yako.

8. Usiweke Simu Yako Sehemu iliyo Jibana au Yenye Joto Kali

Najua fashion bado ni sehemu kubwa ya maisha yetu na watu wengi sana siku hizi huvaa nguo zinazobana sana, kama tunavyojua hauwezi kuacha simu yako hata kama umevaa nguo inayobana hivyo hii husababisha simu yako kukaa kwenye mfuko unaojibana hasa kwa wanaume na kuweza kufanya simu yako kupata joto sana hasa pale unapotembea. Kitu cha muhimu basi ni kuhakikisha beba begi ambalo unaweza kuweka simu yako hata kama utakuwa unasafari ndefu ya kutembea au kazi mbalimbali.

9. Simu Kupata Joto Sana ni Dalili ya Battery Kufa

Kama umefuata hatua zote hapo juu na bado simu yako inapata joto sana basi ni lazima hii ni dalili ya kwanza inayoonyesha kuchakaa kwa battery ya simu yako. Ni vizuri kufuata hatua za kuweza kulinda battery ya simu yako mara tu unapo nunua simu yako ili kuepuka matatizo kama haya. Pia unaweza kutumia baadhi ya app ambazo zinaweza kukusaidia kupunguza joto kwenye simu yako.

Na hizo ndio hatua ambazo zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuondoa tatizo la simu yako kupata moto mara kwa mara, kama unatumia simu ya Tecno unaweza kusoma hapa njia za kufanya simu ya Tecno kudumu na chaji. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea channel ya Tanzania Tech ili kujifunza maujanja mengi zaidi kwa vitendo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use