Mtandao wa Instagram hivi karibuni umetangaza mabadiliko mapya ya vigezo na masharti yake ya matumizi kwa kuleta sheria mpya ambayo itakuwa inawabana watumiaji mbalimbali wa mtandao huo.
Sheria hiyo mpya ambayo imeanza kutumika hivi karibuni, inasababisha watumiaji wa mtandao huo ambao hupata follower pamoja na like kwa kutumia programu mbalimbali kuondolewa like hizo moja kwa moja. Inasemekana kuwa Instagram imebuni mfumo wa mpya wa machine learning, mfumo ambao utakuwa unatumika kuondoa like, follower pamoja na comment zote ambazo akaunti yoyote imepata kwa kutumia programu mbalimbali tofauti na Instagram.
Mbali na hayo inasemekana kuwa instagram itawalazimisha watumiaji wa programu hizo mbalimbali za kuongeza like au followers kubadilisha neno la siri ili kuweza kuongeza ulinzi zaidi kwenye akaunti hizo. Kwa sasa zoezi la kuondoa like pamoja na follower feki bado halijaanza rasmi ila kwa mujibu wa instagram inasemekana zoezi hilo linategemewa kuanza wiki ijayo.
Facebook kwa pamoja na Instagram kwa sasa imekuwa kwenye hatua ya kupambana na akaunti feki kwani wiki hii Facebook iliripoti kuwa ndani ya kipindi kizima cha mwaka huu 2018, imefanikiwa kuondoa akaunti zaidi ya bilioni 1.5 kutoka kwenye mtandao wa Facebook pekee. Kwa upande wa Instagram facebook imedai kuwa imeshagundua akaunti nyingi feki na siku za karibuni itaenda kuchukua hatua ya kuzifuta moja kwa moja kutoka kwenye mtandao huo.
Kama bado unatumia app mbalimbali kwaajili ya kujipatia follower, like pamoja na comment ni vyema sasa kuanza kutumia app ya Instagram yenyewe kwani huanda hivi karibuni Follower hao waka ondoloewa kutoka kwenye akaunti yako.