Ikiwa bado hapa kwetu Tanzania tunajitahidi kukimbizana na teknolojia kwa kuanza kutengeneza simu, huko nchini China wao wanazidi kukuwa kiteknolojia kila siku kwa kuwa wakwanza kuanzisha teknolojia mpya mbalimbali.
Kuthibitisha hayo hivi karibuni kampuni moja Royal ya nchini China imetangaza kuingiza sokoni simu mpya inayoitwa FlexPai ambayo itakuwa ni simu ya kwanza ya namna hii kuingia sokoni ambayo itakuwa na uwezo wa kujikunja na kuwa simu ya kawaida na pia vilevile inaweza kuwa tablet.
Mbali ya kuwa simu ya namna hii, simu hii pia ni ya kwanza kabisa kuja na aina mpya ya processor ya Snapdragon 8150 ambayo inakuja na uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi mbalimbali pale unapokuwa simu na pale inapokuwa tablet. Simu hii inakuja na kioo cha AMOLED ambacho pale kinapokuwa simu kinakuwa na inch 7.8 pamoja na uwiano wa 4:3.
Simu hii inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128, lakini pia inakuja na machaguo mengine ya RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 256 na simu nyingine inakuja na RAM ya GB 8 na ukubwa wa ndani wa GB 512. Mbali na hayo FlexPai pia inakuja na kamera mbili kwa mbele ambazo kamera hizo moja inakuja na Megapixel 16 na kamera nyingine inakuja na Megapixel 20 ambayo hii ni telephoto lens.
Simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa Yuan ya China CNY 9,000 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania 2,972,000 bila kodi. Unaweza kuipata simu hii kwa kutoa oda kupitia tovuti hapa.